Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wale wazee wa muvi hili hapa chimbo la maana

MOVIE Pict

Muktasari:

  • Hapa tutakuwa tukichambua kwa ufupi muvi ya wiki, kisha kukupa orodha ya mzigo wa kuburudika nao wikiendi nzima.

EBWANAEE wikiendi ndo imeanza hivyo. Kwa wale wapenzi wa muvi, tuwe tunakutana hapa kila Ijumaa kupeana vituz.

Hapa tutakuwa tukichambua kwa ufupi muvi ya wiki, kisha kukupa orodha ya mzigo wa kuburudika nao wikiendi nzima.

Pia tutakupa orodha ya kazi zinazotarajiwa kuachiwa ndani ya mwezi, hili mshkaji ujiandae kuzipokea kiroho safi na kuburudisha nafasi. Twende kazi...!


MUVI YA WIKI SAFE

MCHIZI ana moyo wa chuma na shujaa mkimya, akiwa askari wa zamani na mkali wa mapigano (MMA), Luke Wright maisha yanamtibukia baada ya kukataa kushiriki pambano lililopangwa. Mafia wa Kirusi wanapandwa na hasira naye na kumpokonya kila alichonacho akiwamo mkewe, lakini wakasahau ujuzi alionao. Katikati ya wenge hilo anaibuka binti mdogo wa Kichina, Mei mwenye akili na memori kuliko Kompyuta wanayetaka kumtumia katika dili haramu la fedha.

Namba moja ya siri aliyonayo inamweka Mei pabaya kuanzia kwa Wachina wenzie hadi mafia wa Kirusi na Polisi wasio waaminifu wakikichafua kitaani, kila mmoja akiwa tayari kumwaga damu ili wamnase, ila bahati inamkutanisha na Luke aliyejitosa kumsaidia kwa jasho na damu na hapo ndipo uhondo mzima wa dude hili la mwaka 2012 unaponoga.

Filamu hii iliyoongozwa na Boaz Yakin, imechezwa na Jason Statham (Luke Wright), Catherine Chan (Mei), Chris Sarandon (Mayor Tremello), Robert John Burke (Captain Wolf), James Hong (Han Jiao), Matt O’Toole (Detective Lasky) na wengine.

Ngoma hii ina dakika 94 zenye unyama mwingi wa mapigano na ubabe inaishia kwa kuonyesha nafasi ya pili ya maisha kwa Luke na Mei baada ya kutia mtonyo wote ndani. Tukutane wiki ijayo.


MZIGO WA WIKIENDI

Wikiendi ina mambo mengi na kama unataka kuifurahia wikiendi yako freshi ni vyema ukazitafuta hizi muvi tano ili usuuze roho yako!

1. Carry On

2. Assassin Club

3. One Night in Bangkok

4. Perfume

5. The Hitman's Bodyguard


TANO ZIJAZO

Kama una mzuka mwingi wa kusubiri muvi mapya ndani ya Novemba, basi wala usikonde. Hapa chini ni orodha ya filamu tano zitakazoachiwa mwezi huu.

1. Sisu: Road to Revenge- Nov 21

2. Wildcat- Nov 25

3. Blood Star- Nov 25

4. Wake Up Dead Man- Nov 26

5. Eternity- Nov 26


MKALI WA WIKI

Angelina Julie

Kuzaliwa: Jun 04, 1975

Mahali: Los Angeles, Marekani

Fani: Uigizaji, Mtayarishaji

Tangu: 1982

Kazi zake: Salt, Original Sin, Maleficent, Mr& Mirs Smith, The Fever, Tomb Raider, Hackers, Without Evuidence na nyingine.