Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Video ya Mr II Sugu iliyogharimu Sh20 milioni

Muktasari:

  • Tangu miaka ya 1990, Mr. II Sugu alisafari nchi mbalimbali kuutangaza muziki wake na hata kurekodi, hatua iliyompa uzoefu wa kutosha kuhusu muziki. Fahamu zaidi.

JINA la Mr. II Sugu halipo katika orodha ya waanzilishi wa Bongofleva, lakini amecheza nafasi kubwa katika kurasimisha muziki huo na kuwa biashara rasmi, kitu ambacho anajivunia hadi sasa.

Tangu miaka ya 1990, Mr. II Sugu alisafari nchi mbalimbali kuutangaza muziki wake na hata kurekodi, hatua iliyompa uzoefu wa kutosha kuhusu muziki. Fahamu zaidi.

1. Mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 25, ndipo Sugu alifanya show yake ya kwanza barani Ulaya ambapo alitumbuiza nchini Uholanzi, na hii ni moja ya nchi ambazo amezitembelea mara nyingi.

2.Albamu yote ya Sugu inayokwenda kwa jina la Nje ya Bongo ilirekodiwa  Ulaya, mjini Utrecht, Uholanzi mwaka 1999 chini ya producer  Mholanzi. Albamu hiyo ndiyo yenye nyimbo kama Ni Ndoto, Deiwaka na Niko Fresh zilizofanya vizuri zaidi.

3. Nje ya Bongo (1999), inatajwa kuwa  albamu ya kwanza ya 'Muziki wa Kizazi kipya' nchini kurekodiwa Ulaya, ukiacha ya Marehemu James Dandu aliyekuwa akiishi na kurekodia Sweden.

4. Mbali na Nje ya Bongo (1999), Sugu ametoa albamu nyingine kama Mimi (1995), Ndani ya Bongo (1996), Niite Mr II (1998), Millennium (2000), Muziki na Maisha (2001), Itikadi (2002), Sugu (2004), Coming of Age - Ujio Wa Umri (2006) na VETO (2009).

5. Katika albamu yake, Niite Mr II (1998), kuna wimbo unaitwa 'Zaidi Na Zaidi' ambao akimshirkisha mwanamuziki kutokea nchini Denmark, Jokeren, ambaye pia aliweka wimbo huo katika albamu yake.

6. Mwaka 2002, Sugu na Dola Soul walitumbuiza katika tamasha la Mundial, mjini Tilburg, Uholanzi, ambapo alikuwa walikuwa pamoja na wasanii wengi wa Afrika akiwemo Baaba Maal wa Senegal.

7. Albamu ya 10 na mwisho kutoka kwa Sugu, VETO (2009) yenye nyimbo 10, ilitayarishwa huko Brooklyn, Marekani katika studio ya S&S chini ya Puzo na Stigo.

8. Video ya wimbo wake, Hold On (2009) akimshirkisha Andre, ilifanyika New York, Marekani, na iligharimu Dola8,000, wastani wa Sh20.8 milioni kwa sasa.

9. Hold On ndio ulikuwa wimbo wa kwanza kuachiwa kwa ajili ya kuitambulisha albamu ya VETO (2009) ambayo ilizinduliwa Desemba 26, 2009 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

10. Mwaka 2001 akiwa bado hajaanza kuitwa Sugu, Mr II tayari likuwa ni msanii mwenye Business card. Email iliyokuwa kwenye card hiyo ilisomeka [email protected], utakumbuka Deiwaka ni wimbo pia wa msanii huyo.