Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uwoya afichua kutinga na suti, red carpet Bodi ya Filamu

UWOYA Pict

Muktasari:

  • Mastaa hao ambao wanatajwa kuwa miongoni mwa waigizaji wa kundi la A-List, walifika katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania wakiwa wamevalia suti na kujipamba, huku wakiwa wamekuja pia na zulia jekundu waliloliteremsha nje ya ofisi hiyo.

BAADA ya waigizaji wakongwe Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Aunt Ezekiel na Kajala Masanja kuitwa na Bodi ya Filamu Tanzania kuhusu maadili katika kipindi chao cha A-List, ujio wao kwenye ofisi za Bodi hiyo Septemba 7, 2026 umeibua stori nyingine kutokana na namna walivyotinga.

Mastaa hao ambao wanatajwa kuwa miongoni mwa waigizaji wa kundi la A-List, walifika katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania wakiwa wamevalia suti na kujipamba, huku wakiwa wamekuja pia na zulia jekundu waliloliteremsha nje ya ofisi hiyo.

Baada ya kushuka kwenye magari yao, walipita juu ya zulia hilo kuelekea ndani, jambo lililofanya ujio wao uonekane tofauti na ilivyozoeleka kwa mtu anayekwenda kuitikia wito wa taasisi.

UWO 01

Akizungumza na Mwanaspoti, Uwoya amesema suala la wao kuvaa suti halikuwa na uhusiano na wito wa Bodi ya Filamu, bali ni utanashati wao wa kawaida.

“Suti ni utanashati tu. Sisi siku zote huwa smart, sio kwamba tumevalia suti kwa sababu tumeitwa sehemu kama baadhi ya watu wanavyodai,” amesema Uwoya.

Uwoya ameongeza kuwa, kuitwa sehemu yoyote hakumaanishi mtu anatakiwa kwenda akiwa katika hali isiyokuwa nadhifu, akisisitiza kuwa wao hupenda kuonekana smart.

“Sio sababu tumeitwa sehemu basi twende kinyonge, yaani wachafu,” amesema.

Mwanaspoti lilipomuuliza pia kuhusu zulia jekundu walilokuja nalo na kulitandaza kabla ya wao kupita juu yake baada ya kushuka kwenye magari, Uwoya hakutoa maelezo marefu, badala yake, alicheka na kusema aachwe.

UWO 02

Wito huo wa Bodi ya Filamu ulifanyika Septemba 7, 2026 ambapo Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo, Dk Gervas Kasiga, amesema mastaa hao waliitwa kupewa onyo na kukumbushwa wajibu wao kama waigizaji wakongwe, hasa kwa kuzingatia kuwa wanaonekana na vijana wanaoweza kujifunza kutoka kwao.

Kwa mujibu wa Kasiga, baadhi ya maeneo yanayoonekana katika kipindi cha A-List hayakuwa na maadili yanayostahili, hivyo Bodi ikaona ni muhimu kuwakumbusha mastaa hao kutumia nafasi yao kujenga tasnia na kuwa mfano kwa wasanii wanaochipukia.

UWO 03

A-List ni kipindi kinachowakutanisha Uwoya, Wolper, Aunt Ezekiel na Kajala, ambapo huzungumza kuhusu maisha yao, urafiki, kazi na mambo mbalimbali yanayowahusu.

Sasa, wakati suala la maadili likiwa limefika mezani kwa Bodi ya Filamu, ujio wao wa suti, mapambo na zulia jekundu umeongeza stori nyingine pembeni ya kikao hicho.