Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbosso afunguka kuhusu Uwoya

MBOSSO Pict

Muktasari:

  • Mwonekano wao wa pamoja umefufua tena simulizi iliyoanza mwaka mmoja uliopita na mashabiki wengi waliwahusisha na uhusiano wa kimapenzi kutokana na ukaribu wao kwenye matukio mbalimbali na namna walivyokuwa wakipeana sapoti katika mitandao ya kijamii.

UKARIBU wa mwanamuziki Mbosso na mwigizaji Irene Uwoya umeibua tena mjadala baada ya wawili hao kuonekana pamoja mwishoni mwa wiki katika hafla ya A-List iliyowakutanisha mastaa mbalimbali wa Bongo, akiwemo Kajala Masanja, Jacqueline Wolper na Aunt Ezekiel.

Mwonekano wao wa pamoja umefufua tena simulizi iliyoanza mwaka mmoja uliopita na mashabiki wengi waliwahusisha na uhusiano wa kimapenzi kutokana na ukaribu wao kwenye matukio mbalimbali na namna walivyokuwa wakipeana sapoti katika mitandao ya kijamii.

Tetesi hizo zilianza kushika kasi Julai mwaka 2025, baada ya wawili hao kuonekana mara kwa mara wakiwa pamoja. Wakati huo, vyombo mbalimbali vya habari za burudani viliandika kuhusu ukaribu wao, huku mashabiki wakitafsiri huenda urafiki wao ulikuwa umeingia hatua nyingine.

MBO 01

Katika kufuatilia ukweli wa taarifa hizo, Mwanaspoti lilizungumza na Irene Uwoya ambaye alikanusha kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi kati yake na Mbosso na urafiki wao ulikuwepo kwa muda mrefu, isipokuwa watu ndiyo walikuwa wameuchelewa kuugundua.

"Kitu ambacho watu wengi hawakijui, mimi na Mbosso ni marafiki wa muda mrefu na kila mmoja ni shabiki wa mwenzake katika kazi zetu, hakuna kitu kingine na hakitawahi kutokea," amesemaUwoya.

Kwa upande wake, Mbosso aliweka wazi jinsi anavyomthamini mwigizaji huyo, akisema:

MBO 02

"Kwanza nashukuru sana kupata rafiki mwenye upendo wa dhati, Irene Uwoya ni dada mwenye upendo sana."

Licha ya kauli hizo, ukaribu wao uliendelea kuvuta hisia za mashabiki. Wikiendi iliyopita, walipoonekana tena kwenye hafla ya A-List, wengi walirejea kujadili uhusiano wao, jambo lililomfanya Mbosso kufafanua kwa mara nyingine kuhusu uwepo wake katika hafla hiyo.

"Irene Uwoya ni rafiki yangu sana, ndiye aliyenialika kwenye A-List. Kama ningeambiwa nichague yeyote ndani ya A-List, ningemchagua Irene kwa sababu ya urafiki wetu," amesemaMbosso.

MBO 03

Kauli hiyo inaonekana kuendeleza msimamo ambao wawili hao wamekuwa nao tangu walipoanza kuhusishwa mwaka 2025, wakisisitiza kilichopo kati yao ni urafiki wa muda mrefu licha ya mashabiki kuendelea kutoa tafsiri tofauti kila wanapoonekana pamoja.

Hadi sasa, hakuna kati yao aliyewahi kuthibitisha kuwa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwenzake. Hata hivyo, kila wanapokutana kwenye matukio ya kijamii au kuonekana pamoja hadharani, mjadala kuhusu ukaribu wao huibuka upya na kuendelea kuwavutia wadau wa burudani.