Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usaliti, migogoro... Nandy Billnas miaka 4 bado wapo pamoja

NANDY Pict

Muktasari:

  • Wawili hao waliofunga ndoa Julai 16, 2022, katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Julai 18, 2026 wamefanya sherehe nyumbani kwao ya kifamilia kuadhimisha miaka minne ya ndoa yao, wakionesha kuwa bado wanaendelea kushikamana licha ya changamoto mbalimbali.

KATIKA ulimwengu wa burudani ambako ndoa nyingi za mastaa zimekuwa zikivunjika ndani ya muda mfupi, wanamuziki wa Bongo Flava, Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ na mumewe William Nicholaus Lyimo ‘Billnass’, wameendelea kuwapa matumaini mashabiki wao baada ya kutimiza miaka minne ya ndoa.

Wawili hao waliofunga ndoa Julai 16, 2022, katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Julai 18, 2026 wamefanya sherehe nyumbani kwao ya kifamilia kuadhimisha miaka minne ya ndoa yao, wakionesha kuwa bado wanaendelea kushikamana licha ya changamoto mbalimbali.

Safari yao imekuwa ya kupanda na kushuka, ikigubikwa na tetesi za usaliti, migogoro ya kimapenzi na madai ya kutaka kuachana. Hata hivyo, wameendelea kuonyesha kuwa upendo, uvumilivu na mawasiliano vinaweza kushinda vikwazo vingi.

NAND 03

WALIVYOKUTANA

Nandy na Billnass walikutana kupitia shughuli za muziki na kujenga urafiki uliokuja kuzaa mapenzi. Ushirikiano wao katika nyimbo mbalimbali uliwafanya mashabiki wengi kugundua ukaribu wao, kabla ya baadaye kuthibitisha kuwa walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Mwaka 2020, Billnass alimvisha Nandy pete ya uchumba mbele ya familia na marafiki wa karibu.

NAND 02

TETESI ZA KUACHANA

Hata hivyo, mwaka 2021 ukawa mmoja wa miaka migumu zaidi katika uhusiano wao.

Katika kipindi hicho, mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari vya burudani viliripoti kuwa wawili hao walikuwa wameachana baada ya kutofautiana kwenye uhusiano wao.Nandy mwenyewe aliwahi kukiri katika mahojiano kuwa kulikuwa na kipindi ambacho walikuwa wamepeana nafasi (br eak) ili kila m moja atafakari kuhusu mustakabali wa uhusiano wao.

Kwa upande wake, Billnass aliwahi kueleza kuwa si kila kinachoandikwa mitandaoni huwa ni kweli, huku akisisitiza kuwa watu wengi walikuwa wanatafsiri vibaya mambo yaliyokuwa yanaendelea katika maisha yao binafsi.

NAND 01

USALITI NA MIGOGORO

Mbali na madai ya kuachana, kipindi hicho pia kilitawaliwa na tetesi za usaliti ambazo zilienea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.

Ingawa hakukuwa na uthibitisho wa wazi kutoka kwa Nandy au Billnass kwamba mmoja wao alimsaliti mwenzake, uvumi huo uliendelea kuzua mijadala mikubwa, huku mashabiki wakigawanyika kuhusu hatima ya uhusiano wao.

NAND 06

HARUSI

Baada ya kupitia kipindi hicho kigumu, Julai 16, 2022, Nandy na Billnass walifunga ndoa ya kifahari katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Harusi hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa muziki, viongozi wa dini, ndugu na marafiki, huku wengi wakisema ilikuwa ndiyo jibu kwa wale waliokuwa wakiamini kuwa wawili hao wasingeweza kufika madhabahuni.

NAND 05

MIAKA MINNE BAADAYE

Katika kuadhimisha miaka mi nne ya ndoa yao, Nandy alimwandikia mume wake uju mbe uliojaa hisia na shukrani.

“Happy Anniversary my love. Kama masihara miaka minne sasa. Asante kwa kunipa heshima ya kuwa mke wako. Ahadi yangu kwako ni kuendelea kuwa mwanamke unayemtamani ilimradi uwe na furaha. Sala ndiyo nguzo pekee ya ndoa yetu, nitapiga goti mpaka siku naingia kaburini.”

Kauli hiyo imepokelewa na wengi kama ushahidi kuwa imani na sala zimekuwa sehemu muhimu ya maisha yao ya ndoa.

Billnass naye hakusita kumjibu mke wake kwa ujumbe wa mapenzi ulioonyesha jinsi anavyoithamini familia yao.

“Miaka minne au hata miaka elfu nne, nitaendelea kukupenda milele. Happy Anniversary, mke wangu.”

NAND 04

SIRI YAO

Katika kipindi ambacho ndoa nyingi za mastaa zimekuwa zikivunjika kutokana na presha ya umaarufu, migogoro na hukumu za mitandaoni, Nandy na Billnass wameonekana kuchukua njia tofauti.

Badala ya kujibu kila uvumi unaoibuka, wamekuwa wakichagua kutatua changamoto zao ndani ya familia. Mara kadhaa wameeleza kuwa mawasiliano,  uvu

mil ivu, kusameheana na kumweka Mungu mbele ndivyo vimekuwa nguzo ya ndoa yao.

Miaka minne ya safari yao wamemua kupigania ndoa yao badala ya kuiacha ivunjike.