Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TUONGEE KISHKAJI: Amber Lulu, Lamata wanafeli hapa

NAPITAPITA Instagram mara nakutana na video na picha za Amber Lulu, nasimama, naziangalia, naona uso wake umechafuka, sio kwa make up, hapana, kwa majeraha na makovu.

Nasoma caption yake, nagundua makovu na majeraha yote hayo ameyapa kutokana na kipigo alichoshushiwa na mpenzi wake, baba wa mtoto wake.

Kumbukumbu zangu zinanimbia hii sio mara ya kwanza kuona picha za Amber Lulu za aina hii. Na wala sio mara ya kwanza kusikia stori za kwamba mshikaji wa Amber Lulu ana mkono mwepesi, anambonda dada yetu, anampiga kama ngoma, sijui ana mpango naye gani.

Naendelea kusoma caption, nagundua safari hii Amber Lulu ameposti kwa ajili ya kuomba msaada kwa hiki anachopitia. Nashindwa kuelewa, Amber Lulu anaomba msaada Instagram kivipi? Kwanini?

Haiwezekani upigwe, iwe na mwanaume na mwanamke, sura imekuwa kama yule ndege wanamuita kanga, imejaa madoamadoa, lakini unakimbilia Instagram kuomba msaada, kivipi? Instagram ni polisi? Instagram ndio dawati la jinsia? Au matatizo ndo yanatumika kama mtaji wa kutrend na kupush ngoma na majina yenu.

Nachoka stori za Instagram, naingia Youtube kusikilikiza intavyuu, nachagua kusikiliza intavyuu ya Leah Mwendamseke a.k.a Lamata, muongoza filamu mkubwa zaidi Tanzania kwa sasa, ameongeza tamthiliya ya Kapuni na sasa anabamba na tamthiliya ya Jua Kali.

Mwandishi anamuuliza swali ambalo linamchochea Lamata kujibu kwamba kwenye safari yake ya kisanii aliwahi kukutana na tukio la kutaka kubakwa, tena alitaka kubakwa na mtu ambaye ni msanii mkubwa lakini hakutaka kumtaja jina.

Anasema ilikuwa hivi, walikwenda kwenye kambi kushuti filamu, ilipofika usiku, akiwa amelala, huyo staa akamfuata chumbani kwake na kutaka kumfanyia vibaya, akapiga kelele kuomba msaada. Watu wakaja kumsaidia.

Mwandishi anamuuliza, uliwahi kuripoti, anasema hapana, kwa sababu alikuwa anaogopa, alikuwa ni msanii mdogo.

Mwandishi anamuuliza, sasa umeshakuwa msanii mkubwa, una plan ya kumshitaki? Lamata anasema hapana, anamuachia Mungu.

Nilichopenda Lamata hajawahi kuitumia hiyo kama kiki, lakini hiyo haimfanyi kuwa bora kuliko Amber Lulu, kwa sababu alichofanyiwa Amber Lulu akanyamaza, na alichofanyiwa Lamata na akamuachia Mungu yote ni kutowatendea haki masista zetu.

Masista zetu mtaani wanawatazama hawa watu, na masista zetu mtaani wanakutana sana na haya matatizo ya ubakaji na vipondo. Lakini wengi hawafanyi kitu kwa sababu wanaogopa au hawajui cha kufanya, wanamuachia Mungu.

Kwahiyo mastaa wetu, kina Lamata na Amber Lulu ndio walitakiwa kuwa mfano. Lamata angechukua au akichukua hatua kwa alichofanyiwa, atakuwa amesaidia kuwatoa uoga kwa kiasi kikubwa masista zetu ambao wamefanyiwa sana hayo mambo. Pengine atasaidia kuwafanya nao waanze kuwachukulia hatua wabaya wao.