Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wabongo wamlilia Dolly Parton

Muktasari:

  • Dolly alizaliwa Januari 19, 1946, katika eneo la Sevier County, Tennessee, Marekani, akiwa ni mtoto wa nne katika familia ya watoto 12.

BAADHI ya Watanzania  wamesikitishwa na kifo cha mwanamuziki Dolly Parton, kili-chotokea juzi, Agosti 25, 2026, huku sababu ya kifo chake ikielezwa alikuwa aki-sumbuliwa na saratani kwa muda mrefu.

Dolly alizaliwa Januari 19, 1946, katika eneo la Sevier County, Tennessee, Marekani, akiwa ni mtoto wa nne katika familia ya watoto 12.

Miongoni mwa waliosikitishwa na kifo cha mwanamuziki huyo ni mtangazaji maarufu Meena Ally, ambaye amesema atamkumbuka kwa mengi, hasa kupitia nyimbo zake zilizogusa hisia za wengi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Meena amesema Dolly hakuwa tu mwanamuziki, bali pia alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa na aliyekuwa na upendo kwa watu wote.

“Dolly Parton siyo tu mwanamuziki, alikuwa na ushawishi kutokana na maneno yake. Mimi ni mmoja wa wale waliopenda kusikiliza maneno yake. Kama alivyowahi kusema, ‘Ukitaka mafanikio makubwa, lazima upitie changamoto kadhaa katika kupata mafani-kio hayo,” amesema Meena, ambaye ni mdau mkubwa wa muziki nchini.

Mbali na mtangazaji huyo, mchekeshaji Ester Luckson (Mama Chanja), pia al-imzungumzia Dolly Parton, akisema ni miongoni mwa wasanii waliomvutia sana kuto-kana na tungo zake mbalimbali.

“Mimi ni mpenzi wa country songs. Miongoni mwa nyimbo za Dolly nilizokuwa napen-da kusikiliza ni Coat of Many Colors, Jolene na I Don’t Believe You’ve Met My Baby. Hizo ni baadhi tu ya nyimbo nilizokuwa napenda sana kutoka kwa Dolly Parton,” amesema msanii huyo.

Kwa upande wake, mshereheshaji Godfrey Deogratius (MC GaraB) amesema amepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa kutokana na umahiri wa msanii huyo, ambaye amekuwa maarufu kwa muda mrefu.

“Nilikuwa nikisikiliza nyimbo zake nikiwa bado mdogo sana. Kifo chake kimeleta ma-jonzi kwangu. Alikuwa mwanamke ambaye hakubagua watu wa hali yoyote, iwe masi-kini au watu weusi,” amesema MC GaraB, ambaye ni mmoja wa watu maarufu nchini.

Akizungumzia jinsi anavyomfahamu Parton, mhariri wa burudani wa gazeti la Mwananchi, Cristina Joseph (Tinana), amesema Dolly alikuwa mwanamuziki mwenye mashabiki wengi nchini na kifo chake kimewagusa wengi.

Amesema pamoja na muziki, Parton alikuwa miongoni mwa watu waliofanya mambo makubwa, ikiwa ni pamoja na kujenga Dollywood, sehemu ambayo watu wengi wamekuwa wakipata ajira, ikiwa ni moja ya njia zake za kurudisha kwa jamii.

“Dolly alikuwa mtu wa kusaidia watu waliokuwa na uhitaji, ikiwa ni pamoja na ajira, huko nchini kwao Marekani. Pia alianzisha programu kubwa ya elimu inayosambaza mamilioni ya vitabu bure kwa watoto duniani kote ndiyo maana unaona hata familia yake inataka watu wapeleke fedha kwa ajili ya kusapoti hili kuliko maua, nafikiri ni funzo pia kwa familia nyingine,” amesema Cristina.

Parton alifariki akiwa Nashville, Tennessee, huku familia yake ikiwaomba mashabiki, badala ya kutuma maua, wachangie mpango wake wa kutoa vitabu kwa watoto, Dolly Parton’s Imagination Library.

Mwanamuziki huyo, wakati wa uhai wake, alipokea tuzo 11 za Grammy, akiwa mion-goni mwa wasanii wenye ushawishi mkubwa duniani.

Hadi jana jioni familia yake ilikuwa bado haijatoa taarifa kuhusu lini na wapi mazishi yake yatafanyika.