Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri nyuma ya Rich Mavoko

Rich Mavoko.

Muktasari:

  • Yaani ishu ya Rich Mavoko ambaye alijiunga na WCB mwaka 2016 akiwa msanii wa tatu kusaini na lebo hiyo baada ya Harmonize na Rayvanny, inavuma kinoma na huko kwenye mitandao ya kijamii watu wanatokwa povu tu huku kila mmoja akisema imebaki stori.

ACHANA na wimbo wake mpya wa Happy, ambao unatrend kwa sasa kwenye redio na mitandaoni, ishu inayovuma kwa sasa ni Rich Mavoko kuitema Wasafi Classic Baby (WCB).

Yaani ishu ya Rich Mavoko ambaye alijiunga na WCB mwaka 2016 akiwa msanii wa tatu kusaini na lebo hiyo baada ya Harmonize na Rayvanny, inavuma kinoma na huko kwenye mitandao ya kijamii watu wanatokwa povu tu huku kila mmoja akisema imebaki stori.

Iko hivi. Wakati Richard Martin a.k.a Rich Mavoko akijiunga na WCB ambako amefanya kazi kibao zikiwemo kolabo matata kama ya ‘Zilipendwa’ ambayo ilibamba kinoma, mashabiki wengi walipigwa butwaa na wengine wakihoji uamuzi wake huo, wakisema amebugi kinoma.

Hata hivyo, wengine walipongeza wakisema kuwa amekwenda kujiunga na lebo yenye wasanii wanaojitambua na wanaoamini katika kufanya kazi, hata hivyo staili yake ya uimbaji ilielezwa kuwa ni tatizo kwani inafanana kabisa na ya Diamond (Bosi wa WCB) na hata Harmonize kwa mbali. Hata unaposikiliza hit ya Show Me ambayo ni kolabo yake na Harmonize ni ngumu kuwatofautisha sauti zao.

Taarifa za Mavoko kutemana na WCB zilianza kutrend kama utani vile, ambapo Mwanaspoti limekuwa likifuatilia hatua kwa hatua baada ya tetesi kusambaa kwa kasi. Juni 19, Diamond alizungumza na waandishi wa habari ambapo wasanii wote wa WCB walikuwepo isipokuwa Mavoko.

Lakini, Babu Tale alipoulizwa kutokuwepo kwa Mavoko akadai kuwa alikuwa amebanwa akifanya video ya wimbo wake mpya hivyo, asingeweza.

Hata hivyo, wasanii wa WCB wamekuwa na kawaida ya kushirikiana kama siafu pindi wanapokuwa na jambo lao, ambapo wamekuwa wakivamia kwenye mitandao ya kijamii kutangaza kazi za msanii mwenzao, jambo ambalo limekuwa likiwapa mafanikio makubwa.

Hata hivyo, katika kipindi cha wiki kadhaa ushiriki wa Mavoko kwenye kutoa sapoti kwa wenzake umekuwa mdogo, ambapo haposti wala kutoa maoni tofauti na ilivyokuwa zamani hatua inayoashiria kuwa kuna tifu linaendelea chini kwa chini.

Katika ukurasa wake wa Instagram, mara ya mwisho kwa Mavoko kuposti posti inayohusisha WCB ilikuwa Mei 25, mwaka huu, ambapo aliandika BadMan. Pia, baada ya hapo akaunti yake hiyo haijatoa dalili yoyote kuwa ni mmoja wa wasanii wa lebo ya WCB kama zilivyo za Rayvanny, Hamornize, Lavalava Maromboso na Queen darlin.

Pia, Mavoko amekuwa haonekani kwenye matukio mbalimbali yanayowahusu wasanii wa WCB ikiwemo tangazo la kutangaza kipindi kipya cha Wasafi, jambo ambalo limezidisha utata kuhusiana na uwepo wake ndani ya lebo hiyo inayosumbua kinoma Afrika Mashariki kwa sasa.

Lakini, kama kawaida yake Babu Tale alipoulizwa akadai kuwa Mavoko alikuwa safari kwenda kushiriki msiba wa dada yake nyumbani kwao Kilosa, Morogoro.

“Yaaa Mavoko hayupo kwenye kipande cha video ya Reality Show kwa sababu wakati tunarekodi alikuwa msibani Kilosa, bahati mbaya alipatwa msiba wa dada yake,” alisema.

Timu ya Mwanaspoti ilimsaka Mavoko ili kuzungumzia ishu nzima ya kinachoendelea baina yake na WCB huku pia kukiwa na madai kuwa, ametimuliwa na mabosi zake.

Kwanza Mwanaspoti ilimzukia nyumbani kwake Tabata, lakini ikaelezwa kuwa amehama na makazi yake mapya hayajulikani hivyo, kulazimika kumsaka kwa simu yake ya kiganjani.

Alipopatikana Mavoko alionekana mwenye furaha na kumtaka mwandishi kuwasiliana naye Jumatano ili wapange mahali kwa kukutana, lakini siku ilipowadia hakupokea simu.

Saa chache baadaye alipatikana na kueleza kuwa amebanwa na majukumu hivyo, wanaweza kuzungumza kwa simu lakini, akaweka angalizo kuwa hataki kuulizwa maswali kuhusiana na WCB.

Hata hivyo, akaelezwa kuwa ishu kubwa ni kuzungumzia wimbo wake mpya wa Happy ambao umefanyiwa kazi studio za S2Kizzy na sio Wasafi records, japo masuala ya WCB ni muhimu yakajadiliwa kwa kuwa ndio lebo anayofanyia kazi kwa sasa. Mahojiano yake na Mwanaspoti yalikuwa kama hivi:

Mwanaspoti: Unazungumzia wimbo wa Happy na kwanini umerekodiwa studio za S2Kizzy na sio Wasafi.

Mavoko: Hayo ni maamuzi tu ya wapi ukarekodi, jambo la msingi naomba sapoti.

Mwanaspoti: Tangu umeachia huu wimbo, mbona hakuna msanii wa WCB aliyeuposti kama ilivyo kawaida yenu?

Mavoko: Hilo ni vizuri ukawauliza wahusika ndio watakuwa na majibu sahihi.

Mwanaspoti: Kuna taarifa kuwa umeondoka WCB, habari hizi zina ukweli kiasi gani

Mavoko: Nilishakwambia sitaki kuzungumzia WCB, wewe watafute viongozi wa WCB labda ndiyo watazungumza.

Jitihida za Mwanaspoti kuwapata mabosi wa WCB, Babu Tale na Mkubwa Fella hata kupitia simu zao za kiganjani hazikuweza kuzaa matunda kwani, hazikuwa zikipokewa.