Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sinners yamsogeza karibu Jordan katika Oscars

Muktasari:

  • Jordan alitangazwa mshindi wa tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume katika Nafasi ya Kuongoza kwa uigizaji wake katika filamu ya kutisha ya vampaya Sinners, ambayo pia ilishinda tuzo kubwa ya usiku huo ya Waigizaji Bora kwa Pamoja (Best Ensemble Cast).

LOS ANGELES, MAREKANI: MWIGIZAJI wa Marekani, Michael B. Jordan, amepata ushindi wa kushtukiza katika  tuzo za Actor (zamani zikijulikana kama Screen Actors Guild Awards), hali iliyompa nguvu mpya katika wiki za mwisho zikikaribia zile  za Oscars.

Jordan alitangazwa mshindi wa tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume katika Nafasi ya Kuongoza kwa uigizaji wake katika filamu ya kutisha ya vampaya Sinners, ambayo pia ilishinda tuzo kubwa ya usiku huo ya Waigizaji Bora kwa Pamoja (Best Ensemble Cast).

Tuzo hizo zilitolewa Machi Mosi 2026 na sherehe zake zilifanyika Shrine Auditorium and Expo Hall huko Los Angeles.

“Sijui nianzie wapi, sikuitegemea kabisa hii,” amesema Jordan katika hotuba yake, akiongeza alihisi kuheshimiwa na kubarikiwa kuteuliwa kushinda tuzo hiyo.

Akikabidhiwa tuzo ya waigizaji bora kwa pamoja, mwigizaji mwenzake, Delroy Lindo, alisema kutengeneza Sinners ilikuwa safari ya ajabu, akiongeza: “Kila siku tulileta nafsi zetu, mioyo yetu na roho zetu katika kazi hii.”

Lindo aliongeza: “Kutambuliwa na nyinyi, neno ‘asante’ halitoshi kueleza shukrani tunazohisi.”

Tuzo za Sinners zilikuja wiki moja baada ya Tuzo za Filamu za Bafta, ambapo Jordan na Lindo walipongezwa kwa utulivu wao baada ya mwanaharakati wa Tourette’s, John Davidson, kupiga kelele bila hiari akitamka tusi la kibaguzi walipokuwa jukwaani.

Washindi wengine wa Actor Awards ni pamoja na Sean Penn (One Battle After Another), Jessie Buckley (Hamnet), ushindi wa kushtukiza wa Amy Madigan (Weapons) kama mwigizaji bora wa kike msaidizi, pamoja na ushindi wa baada ya kifo wa Catherine O’Hara (The Studio).

Katika hotuba yake ya shukrani, Jordan alimpongeza mama yake Donna, ambaye amekuwa akiandamana naye katika matukio ya msimu wa tuzo, kwa kumuunga mkono tangu akiwa mdogo.

“Mama, asante kwa kuniendesha kwenda na kurudi New York wakati hatukuwa na fedha za kutosha kupita kwenye Harlem Tunnel, tulipokuwa tunatafuta pesa za mafuta na sehemu za maegesho,” alisema.

Jordan pia alimshukuru mkurugenzi wa Sinners, Ryan Coogler, pamoja na waigizaji wenzake, akisema: “Kila aliyeshiriki katika filamu hii, mlitupatia muda wenu, vipaji vyenu na udhaifu wenu na kuniruhusu nitoe kazi yangu bora.”

Upigaji kura wa Actor Awards ulifungwa Ijumaa, siku tano baada ya sherehe za Bafta ambako neno la kibaguzi lilitamkwa jukwaani. Lindo alizungumzia tukio hilo katika hafla nyingine, akisema: “Tunathamini sana msaada na upendo tulioonyeshwa baada ya yaliyotokea. Ni mfano wa jambo ambalo lingeweza kuwa hasi lakini likageuka kuwa chanya.”


CATHERINE O’HARA ASHINDA TUZO BAADA YA KIFO

Nyota wa Home Alone na Schitt’s Creek, Catherine O’Hara, aliyefariki Januari 2026, alitangazwa mshindi wa Mwigizaji Bora wa Kike katika Vichekesho vya Televisheni kwa nafasi yake katika tamthilia ya kejeli ya Hollywood, The Studio.

Akikabidhiwa tuzo kwa niaba yake, muundaji wa kipindi hicho Seth Rogen, alisema: “Alionyesha unaweza kuwa gwiji na pia mtu mwema na vitu hivyo viwili havipingani.”

The Studio pia ilishinda tuzo ya Waigizaji Bora wa Vichekesho na Mwigizaji Bora wa Kiume katika Vichekesho kwa Rogen.

Washindi wengine wa televisheni ni pamoja na Michelle Williams (Dying For Sex), Keri Russell (The Diplomat) na muigizaji wa Uingereza, Owen Cooper (Adolescence).

JESSIE BUCKLEY AENDELEA KUNG’ARA

Nyota wa Hamnet, Jessie Buckley, alisema ni heshima kubwa kushinda tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike, kitengo ambacho amekuwa akitawala msimu huu wa tuzo. Filamu hiyo inasimulia kwa namna ya kubuni kifo cha mwana wa William Shakespeare mwenye miaka 11.

Buckley alimpongeza mwigizaji mwenzake Emily Watson kwa ushirikiano wao, akisema: “Kushiriki nawe katika Hamnet nitakuthamini maisha yangu yote.”


AMY MADIGAN AFUFUA MBIO ZA MWIGIZAJI MSAIDIZI

Kulikuwa na ushindi mwingine wa kushtukiza kwa Amy Madigan, mwenye miaka 75, aliyeshinda kama Mwigizaji Bora wa Kike Msaidizi kwa nafasi yake katika filamu ya kutisha, Weapons.

“Sikutegemea hili, lakini lina maana kubwa sana kwangu kutoka kwa wenzangu,” alisema.

Ushindi wake unampa nguvu mpya kuelekea Oscars baada ya kupoteza kasi katika baadhi ya tuzo zilizotangulia.


HARRISON FORD ATUZWA KWA MAFANIKIO YA MAISHA

Harrison Ford alipokea tuzo ya mafanikio ya maisha baada ya kazi ya zaidi ya miongo sita iliyojumuisha filamu kama Star Wars, The Fugitive, Indiana Jones na Blade Runner.

“Ni ajabu kidogo kupokea tuzo ya mafanikio ya maisha katikati ya kazi yangu,” alitania Ford mwenye umri wa miaka 83.

“Nina bahati kuwa bado nafanya ninachokipenda.”


JE, SINNERS INAWEZA KUSHINDA TUZO YA FILAMU BORA?

Actor Awards hupigiwa kura na waigizaji wenzao na mara nyingi huashiria mwelekeo wa Oscars. Sinners inaingia Oscars ikiwa na uteuzi 16, idadi kubwa zaidi kwa filamu yoyote katika historia ya Academy Awards.

Filamu hiyo, inayotokea katika miaka ya 1930 Mississippi Delta, inasimulia hadithi ya mapacha wawili (waliochezwa na Jordan) wanaotaka kufungua ukumbi wa muziki kabla ya mipango yao kuvurugwa na nguvu ya uovu.

Ingawa Sinners ni mshindani mkubwa wa Filamu Bora, inakabiliwa na ushindani mkali kutoka One Battle After Another, ambayo imeshinda tuzo kadhaa muhimu katika Golden Globes, Bafta na Producers Guild Awards.

Ushindi wa Jordan umefanya mbio za Mwigizaji Bora wa Kiume kuwa ngumu kutabirika kabla ya Oscars, zitakazofanyika Machi 15, 2026, huku washindani wengine kama Timothée Chalamet na Wagner Moura wakiwa pia wamepata ushindi katika hafla nyingine.

Kwa sasa, ushindi wa Jordan umeacha mbio hizo zikiwa wazi kabisa.