Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dakika 57 za moto za Bi Mwanahawa Ally jukwaani

DAKIKA Pict

Muktasari:

  • Dakika hizo 57 jukwaani zimeongeza ukurasa mwingine katika safari ndefu ya Mwanahawa, ambaye ameendelea kutambulika kwa uzoefu wake na mchango wake katika muziki wa Taarab nchini.

LICHA ya kutangaza kustaafu muziki kutokana na changamoto za kiafya, mwanamuziki mkongwe wa Taarab nchini, Bi Mwanahawa Ally, ameonyesha kuwa bado ana mapenzi makubwa na muziki baada ya kutumbuiza kwa dakika 57 katika shoo ya kuadhimisha miaka 20 ya safari ya muziki ya Isha Mashauzi.

Shoo hiyo ilifanyika Super Dome, Masaki, Dar es Salaam, ambako Mwanahawa aliwasili saa 3:28 usiku akishikiliwa mkono na watu wake wa karibu, hali iliyovuta hisia za baadhi ya waliohudhuria.

Muda wa kupanda jukwaani ulipofika, aliandaliwa kiti cha kukaa, lakini hakukitumia. Badala yake, alisimama na kuanza kutumbuiza, akiwapa mashabiki nafasi ya kushuhudia tena burudani kutoka kwa mmoja wa wakongwe wa muziki wa Taarab nchini.

Mwanahawa alipanda jukwaani saa 6:17 usiku na kuanza kwa wimbo Umaskini Wangu, kabla ya kufuatiwa na Viumbe Wazito. Aliendelea kusimama akiimba hadi saa 7:14 usiku aliposhuka jukwaani, akiwa ametumia jumla ya dakika 57 kutumbuiza.

MWANA 01

Kitendo cha kusimama jukwaani muda wote licha ya kuandaliwa kiti kilikuwa miongoni mwa matukio yaliyoifanya burudani yake kuwa ya kipekee. Shoo hiyo pia iliwakutanisha wasanii na mashabiki wa Taarab na Bongo Fleva, huku Zuchu, Mama Mobetto na msanii wa filamu Gabo wakitajwa miongoni mwa waliomtunza kwa fedha.

Mwanahawa alianza safari yake ya muziki mwaka 1966. Hadi mwaka 2026, amekuwa katika tasnia hiyo kwa takribani miaka 60, akishuhudia mabadiliko mbalimbali ya muziki wa Taarab na kujijengea nafasi kama mmoja wa wanamuziki wakongwe nchini.

Hata hivyo, Agosti 20, 2024, Mwanahawa alitangaza kustaafu na kuacha kujishughulisha kikamilifu na muziki. Uamuzi huo ulihusishwa na changamoto za kiafya, zikiwamo matatizo ya miguu yaliyokuwa yakimzuia kutumbuiza kama ilivyokuwa awali.

MWANA 02

Pamoja na uamuzi huo, Mwanahawa amekuwa akijitokeza mara chache katika matamasha maalumu. Ushiriki wake katika shoo ya Isha Mashauzi ni sehemu ya kuendelea kuungana na muziki ambao amekuwa akiufanya kwa takribani miongo sita.

Dakika hizo 57 jukwaani zimeongeza ukurasa mwingine katika safari ndefu ya Mwanahawa, ambaye ameendelea kutambulika kwa uzoefu wake na mchango wake katika muziki wa Taarab nchini.