Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Si Linah na Nandy pekee, kuna hawa pia

Muktasari:

  • Itakumbukwa Linah aliyeibuliwa na Tanzania House of Talent (THT), anakuwa mwanamuziki wa tatu kusainiwa na lebo hiyo baada ya Yammi na Pipi Jojo ambaye ametambulishwa mwaka huu

KWA sasa Linah a.k.a Ndege Mnana atakuwa chini ya usimamizi wa Nandy kimuziki kupitia rekodi lebo ya The African Princess ambayo imejikita kufanya kazi na wanamuziki wa kike pekee.

Itakumbukwa Linah aliyeibuliwa na Tanzania House of Talent (THT), anakuwa mwanamuziki wa tatu kusainiwa na lebo hiyo baada ya Yammi na Pipi Jojo ambaye ametambulishwa mwaka huu.

Linah, mkali wa kibao cha Ole Themba (2014), anasainiwa na Nandy baada ya kuwa kimya kimuziki kwa takribani miaka mitatu. Wimbo wake wa mwisho kuachia unaitwa 'Nyota' ambao ulitoka Desemba 2023 ukiwa umetayarishwa na Jini x66.

Hata hivyo, Linah si mwanamuziki wa kwanza wa Bongofleva ambaye ni maarufu kusainiwa katika lebo ya msanii mwenzake ambaye pia anaweza kuwa hata mshindani wake. Hawa ni wengine.

1. Rich Mavoko & Diamond

Kabla ya kusainiwa WCB Wasafi yake Diamond Platnumz, tayari Rich Mavoko alishakuwa juu kimuziki kwa miaka zaidi ya mitano na waliwahi kuchukuliwa kama washindani.

Mwaka 2016, ndipo akasaini WCB Wasafi akiungana na Harmonize na Rayvanny waliokuwa chini ya lebo hiyo kwa wakati huo, ila Mavoko alikuja kuondoka WCB Wasafi mwaka mmoja baadaye.

Na Rich Mavoko ndiye alikuwa mwanamuziki wa kwanza katika historia kuondoka WCB Wasafi, hatua iliyoleta mgogoro kati ya pande hizo mbili. Inaelezwa hadi sasa chaneli ya YouTube ya Mavoko inashikiliwa kwa kushindwa kumalizika vizuri.

2. AY & Ommy Dimpoz

Rapa AY, mwanachama wa zamani wa kundi la East Coast Team, mwaka 2012, kupitia lebo yake ya Unity Entertainment alimsaini Ommy Dimpoz ikiwa ni mwaka mmoja tangu amevuma kimuziki kwa mara ya kwanza.

Hata hivyo, baada ya muda Ommy Dimpoz aliacha kufanya kazi na Unity Entertainment, na baadaye alianzia lebo yake iitwayo Poz Kwa Poz (PKP) ambayo ilikuja kumtoa kimuziki Nedy Music mwaka 2016 kupitia wimbo wake, Usiende Mbali. Mbali na Ommy Dimpoz, AY pia aliwasaini wasanii wengine kama Stereo ambaye alishatoka chini ya M-Lab, pia na Feza Kessy, mshiriki wa Big Brother Africa Tha Chase 2013.

3. Harmonize & Country Wizzy

Mwaka 2020, kwa mara ya kwanza Harmonize alimtambulisha mwanamuziki ambaye tayari ni maarufu katika lebo yake ya Konde Music Worldwide, naye si mwingine bali rapa Country Wizzy ambaye alianza kuvuma mwanzoni mwa 2010.

Baada ya mwaka mmoja, Country Wizzy aliondoka Konde Music kwa madai mkataba wao umemalizika, kisha akaenda kuanzisha lebo yake, I Am Music ambayo kwa sasa inamsimamia rapa Barbie Mia, na kundi la rap la Fresh Boys. Na Country Wizzy ndiye alikuwa msanii wa kwanza kuondoka Konde Music, kisha wakaja kufuata wengine wanne, kitu ambacho kimeifanya lebo hiyo kwa sasa kutokuwa na mwanamuziki wa kumsimamia.

4. Queen Darleen & Diamond

Akiwa kama ndugu wa Diamond, Queen Darleen alipata kazi ofisi za WCB Wasafi, na baadaye lebo hiyo ilipoanza kuwasaini wanamuziki naye naye akapata fursa hiyo akitambulishwa mwaka 2016. Kolabo yake na Rayvanny, Kijuso (2016) ndio ngoma yake ya kwanza chini ya lebo hiyo, na aliendelea kutoa nyimbo hadi mwanzoni mwa 2020 alipoachana na lebo hiyo na muziki kabisa.

Ikumbukwe Queen Darleen alikuwepo kwenye muziki miaka mingi kabla hata Diamond hajatoka. Aliwahi kusainiwa katika lebo ya G Records ambayo ndio iliyomtambulisha Alikiba kimuziki.

5. Alikiba na Tommy Flavour

Tayari Tommy Flavour alikuwa amejitambulisha kwenye Bongofleva kama mwimbaji mkali wa RnB kupitia kolabo yake na Vanessa Mdee na Maua Sama, Bounce (2017), hivyo Alikiba akaamua kumuongeza katika lebo yake ya Kings Music.

Tommy Flavour alitambulishwa rasmi Kings Music hapo Aprili 2020, na akaendelea kuitambulisha vizuri Kings Music hadi alipokuja kutangaza kuachana na lebo hiyo mwaka uliopita, na sasa anajisimamia mwenyewe kimuziki.

Akiwa Kings Music, Tommy Flavour alishirikiana na Alikiba katika nyimbo tatu, moja ya kati ya hizo ni ule uitwao Huku (2023) ambao ulipokelewa vizuri na sasa ukiwa ni wimbo namba nne wa Alikiba kufanya vizuri zaidi YouTube.