Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Safari ya Chidi Benz

CHID Pict

Muktasari:

  • Kabla hata ya matumizi ya mitandao ya kijamii kushika kasi nchini, tayari Chidi Benz alikuwa na umaarufu mkubwa kupitia muziki wake ambao uliwakosha hata wasanii wenzake waliokuja kumshirikisha kwa wengi. Fahamu zaidi.

RAPA Chidi Benz ni miongoni mwa wasanii wa Hip Hop Bongo ambao muziki wao umeweka alama katika Bongofleva ukiwaburudisha wengi kwa miaka nenda rudi huku pia ukiacha ujumbe muhimu.

Kabla hata ya matumizi ya mitandao ya kijamii kushika kasi nchini, tayari Chidi Benz alikuwa na umaarufu mkubwa kupitia muziki wake ambao uliwakosha hata wasanii wenzake waliokuja kumshirikisha kwa wengi. Fahamu zaidi.


1. Mama mzazi wa Chidi Benz ndiye alimshauri rapa huyo kuutoa wimbo wake, Dar es Salaam Stand Up (2010), basi Chidi akarudi tena studio kurekebisha baadhi ya vitu na ndipo akautoa na ulifanya vizuri sana, hadi sasa ni moja ya nyimbo zake bora kwa muda wote.


2. Ngoma hiyo (Dar es Salaam Stand Up) ilitengenezwa ndani ya studio yake Dully Sykes, Studio 4.12, huku mtayarishaji akiwa Pancho Latino kabla ya kutimkia Bxtra Records, zamani B’Hits Music Group yake Hermy B.

CHI 01

3. Mtayarishaji muziki, Allan Mapigo na Ruge Mutahaba ndio walimtafuta Chidi Benz na kumuomba kushiriki katika wimbo wake Marlaw, Bado Umenuna (2007), hiyo ni baada ya Ruge kuona uwezo mkubwa wa mwimbaji hiyo kufuatia kufanya mazoezi pale THT.

Wakati huo tayari Marlaw alishafanya vizuri na wimbo wake, Bembeleza (2006) aliourekodi akiwa kidato cha sita mkoani Njombe, na wimbo huo ndio ulimtangaza zaidi Prodyuza Tuddy Thomas.


4. Chidi Benz ndiye alikuwa shahidi kipindi Soggy Doggy anasaini makubaliano ya kununua gari lake la kwanza ambalo alitafutiwa na Mwana FA baada ya kupokea Sh6 milioni kama malipo ya mauzo ya albamu yake chini ya Bongo Records.


5. Huyu ni miongoni mwa wasanii wachache Bongo waliofanikiwa kushirikishwa katika nyimbo za washindani wakubwa wawili kimuziki, Diamond Platnumz (Nalia na Mengi) na Alikiba (Far Away), ni kabla wasanii hao kuwa na majina makubwa kama ilivyo sasa.

CHI 02

6. Professor Jay ndiye aliombwa kushiriki katika wimbo wa Tundaman, Neila (2006) ila yeye akampendekeza Chidi Benz ambaye alikuwa na ukaribu naye. Basi Chidi akakubali na kuibuka Baucha Records ambapo Bob Manecky alikuwa anafanya kazi wakati huo.


7. Chidi alipoweka versi yake tu katika wimbo huo ukafanya vizuri na kumtoa kimuziki, baadaye Tundaman akajiunga na kundi la Chid, Lafamilia kisha kutimkia Tip Top Connection baada ya kupewa ofa nzuri na aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo, Abdu Bonge.

Ikumbukwe wimbo huo ndio ulibeba jina la albamu ya kwanza ya Tundaman, Neilah (2007) kisha ya pili, Nipe Ripoti (2009), na ndio uliompa show ya kwanza kulipwa fedha nyingi akichukua Sh400,000 kutoka kwa Promota Bonga ambaye aliwahi kuwa Meneja wa Alikiba.


8. Kupitia wimbo wake, Pisha (2009), Chid Benzi anajitambulisha kama Busta Rhymes wa Tanzania, wakati Gigy Money katika wimbo, Good Time (2018) aliyoshirikishwa na RJ The DJ anajitambulisha kama Cardi B wa Tanzania.

CHI 03

9. Kwa mara ya kwanza Chid Benzi alishinda Tuzo za Muziki (TMA) 2006 kama Msanii Bora wa Hip Hop baada ya kufanya vizuri na wimbo wake ‘Naitwa Nani’ akimshirikisha K-Lynn, Miss Tanzania 2000 na mwimbaji wa zamani wa Tanzanites Band.

K-Lynn ambaye aliachana na muziki baada ya kutoa wimbo, She Ain’t a flirt (2009), alianza muziki mwaka 1997 katika bendi hiyo, aliimba hapo kama msanii na mmoja wa viongozi kwa kipindi cha takribani miaka miwili na nusu.


10. Kipindi Danny Msimamo anarekodi wimbo wake, Siku Nzuri (2004) pale Aigies Records kwa Complex, alikutana na Chid Benzi ambaye alikuwa anatafuta nafasi ya kutoka, kipindi hicho Chid anaimba na sio kurap kama alivyokuja kutambulika.