Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu ya Wema kujitenga ni hii

WEMA Pict

Muktasari:

  • Wema ameliambia Mwanaspoti kuwa, muda umefika wa kuwafungia vioo watu ambao hawana manufaa kwake.

KUMEKUWA na maswali kila uchao kwa msanii wa filamu za kibongo Wema Sepetu, kuhusu kujitenga kwake kwa kushindwa kuhudhuria kwenye sherehe, vikao vya starehe na hata kwa baadhi ya watu wake wa karibu kuwa nao mbali, sasa mwenyewe ametoa sababu.

Wema ameliambia Mwanaspoti kuwa, muda umefika wa kuwafungia vioo watu ambao hawana manufaa kwake.

Alisema Wema, anashangaa mno kuona mtu au watu wanamsema kuwa anaringa, lakini kumbe sivyo hivyo ameamua kudili na watu wenye faida kwake kwa sababu kuna watu wapowapo tu, hata asipowaona hakuna kinachopungua kwake.

“Ni kweli kabisa nimejitenga na baadhi ya mambo na mengine nimeyapunguza wala watu hawakosei kusema hivyo, na hii ni kutokana na kuamua kuwafungia vioo watu ambao hawanisaidii chochote, yaani hawana mchango hata wa mawazo mazuri kwangu, kipindi nashiriki sana starehe, sherehe za bethidei za watu, vikao vya starehe vya marafiki wa kike na wa kiume nilikuwa nafanya mambo ya ajabu sana mengine hayafai katika jamii na sitaki kuyakumbuka.

“Nilidhalilika sana na kushuka thamani yangu, sasa nikaamua kukaa chini kufikiria nainuka vipi ili kutoka huku nilikokua na kwenda nilipo sasa ndio nikaamua kuanza taratibu kupunguza marafiki yaani kupunguza kampani ambazo hazina faida, kupunguza kwenda kwenye masherehe na kuacha starehe na hata pombe kuiacha kabisa maana hii nayo ilikuwa ni kitu kibaya kwangu, nilivyoweza kuepuka hizi mambo ndio nikaamua kuanzisha ‘Wema wa Mama’ ambayo imezidi kuniweka bize sana, nashukuru kwa hill, maana imenifanya kuzunguka mikoa mingi bila kutulia nyumbani Dar es Salaam,” alisema.