Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saa 3 za Fally Ipupa jukwaani, shati lake lazua mjadala

SAA 3 Pict

Muktasari:

  • Fally alipanda jukwaani saa 6 usiku na kuanza burudani kwa wimbo wake maarufu ‘Sweet Life’, uliopokelewa kwa shangwe na mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushuhudia shoo ya nyota huyo wa Rhumba.

MWANAMUZIKI nyota wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Fally Ipupa, ameonyesha ubora wa muziki wa live kwa kutumia saa tatu jukwaani bila kushuka, akitawala burudani kwa sauti, mauno na miondoko yake katika tamasha lililofanyika Lugalo Golf Course, Kawe, usiku wa kuamkia leo Novemba 29, 2026.

Fally alipanda jukwaani saa 6 usiku na kuanza burudani kwa wimbo wake maarufu ‘Sweet Life’, uliopokelewa kwa shangwe na mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushuhudia shoo ya nyota huyo wa Rhumba.

SAA 03

Katika muda wote aliokuwa jukwaani, Fally alionyesha namna mwanamuziki anavyoweza kutoa burudani ya live bila kutumia nguvu nyingi, akitawala jukwaa kwa sauti na miondoko yake, huku wacheza shoo wake na waimbaji wakiongeza ladha kwa kufanya vizuri katika kazi zao.

Ubora wa sauti ulikuwa miongoni mwa mambo yaliyoifanya shoo hiyo kuvutia zaidi, kwani kuanzia mwanzo hadi mwisho, sauti ya Fally, waimbaji wake pamoja na vyombo vya muziki vilisikika vizuri, hali iliyowapa mashabiki nafasi ya kufurahia burudani hiyo bila changamoto yoyote.

SAA 02

Katika kipindi chote cha shoo hiyo, Fally alibadilisha mavazi mara tatu, akianza na shati pana la rangi ya maruni na suruali nyeusi, kisha shati la rangi ya dhahabu na nyeusi lililoambatana na suruali nyeusi. Baadaye alibadilisha tena na kuvaa shati jeupe pamoja na suruali ya rangi ya kijeshi.

SAA 01

Nyimbo mbalimbali alizozitumbuiza zilipokewa kwa shangwe, lakini zilizotikisa zaidi ni ‘May Day’, ‘Eloko Oyo’, ‘Afsana’, ‘Bakanja’ na ‘Associe’, huku mashabiki wakionekana kuimba pamoja naye na kufurahia kila kipande cha burudani.

Hata hivyo, shoo hiyo haikukosa matukio, kwani kuna wakati Fally alisimamisha burudani ghafla baada ya kubaini uwepo wa waya na mchanga jukwaani, akitaka eneo hilo lisafishwe kabla ya kuendelea kutumbuiza. Tukio hilo lilionyesha kutoridhishwa kwake na hali ya maandalizi ya jukwaa.

Mbali na burudani, shati lake la rangi ya maruni (chocolate), lililokuwa pana na kumzidi ukubwa wa kawaida, limekuwa kivutio kwa mashabiki kutokana na namna alivyokuwa akilitumia kucheza, kulipandisha juu na kuzungusha, jambo lililozua shangwe ukumbini na mjadala mitandaoni, baadhi wakilifananisha na mavazi ya wasanii wa vichekesho nchini, Brother K na Leonard pindi wanapokuwa wanaigiza.

Katika matukio mengine ya jukwaani, baadhi ya mashabiki wa kike walipanda stejini kumuomba mwanamuziki huyo kuwakumbatia, jambo lililoongeza msisimko katika tamasha hilo lililohudhuriwa na umati mkubwa wa mashabiki na warembo mbalimbali.