Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rushaynah asisitiza Manara hajaoa, wanawasiliana

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Rushaynah amesema alitoa kauli hiyo kwa sababu swali hilo hakupaswa kuulizwa yeye, lakini pia kutokana na ukaribu wake na Manara, anaamini angejua hata kama ndoa hiyo ingefanyika kwa siri.

Aliyewahi kuwa mke wa ofisa habari wa zamani wa Yanga, Haji Manara, amefafanua kuhusu kauli yake iliyozua mjadala mitandaoni alipodai kuwa Manara hajaoa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Rushaynah amesema alitoa kauli hiyo kwa sababu swali hilo hakupaswa kuulizwa yeye, lakini pia kutokana na ukaribu wake na Manara, anaamini angejua hata kama ndoa hiyo ingefanyika kwa siri.

Katika maelezo yake, Rushaynah amedai bado ana mawasiliano na Manara kiasi cha kujua mambo mengi yanayomhusu.

Amesisitiza kuwa kauli yake haikuwa ya kubahatisha, bali ilitokana na uhalisia wa uhusiano wao wa sasa ambao umejengwa juu ya urafiki.

“Nitasema ukweli, mimi na Haji bado tunaongea sana na tunakutana mara kwa mara. Hivyo suala la yeye kuoa si jambo ambalo linaweza kunipita kirahisi. Kama angeoa hata kwa siri, kwa ukaribu wetu huu ningekuwa najua tu. Ndiyo maana nilisema hajaoa, na si kwa nia mbaya bali kwa kile ninachokijua,” amesema Rushaynah kwa msisitizo.

Ameeleza kuwa licha ya historia yao ya ndoa iliyovunjika, kwa sasa wameweka tofauti zao pembeni na kujenga mahusiano ya kindugu. Hata hivyo, amedai hana mpango wowote wa kurudiana na Manara, lakini pia hana uadui naye, jambo linalowafanya kuendelea kuwasiliana bila tatizo.

“Kwa sasa Haji ni kama ndugu yangu. Tunaongea mambo mengi sana, tunashauriana na hata kusaidiana pale inapobidi. Hakuna chuki kati yetu, lakini pia hakuna suala la kurudiana,” ameongeza.

Kauli ya Manara kwamba ameoa aliitoa mwenyewe mwezi mmoja uliopita katika mahojiano na chombo kimoja cha habari, huku akidai mkewe huyo mpya sio mtu wa mitandaoni.

Manara na Rushaynah walifunga ndoa Septemba 26, 2022 kabla ya kuachana Januari 2023, ambapo Rushaynah alidai kupewa talaka moja.

Tangu hapo, kumekuwa na taarifa mbalimbali zinazowahusisha, ikiwemo madai ya kurudiana kisirisiri yaliyosambaa Julai 2025, lakini kila mmoja amekuwa akikanusha. Licha ya uvumi huo, maelezo ya Rushaynah yanaonyesha kuwa uhusiano umebaki katika msingi wa urafiki na kuheshimiana, huku kila mmoja akiendelea na maisha yake.