Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Riyama, mumewe kumbe hivi!

RIYAMA Pict

Muktasari:

  • Riyama na Mysterio walifunga ndoa Juni 16, 2016 na Juni 2026 wakatimiza miaka 10 ya ndoa yao, licha ya mara kadhaa kuibuka kwa taarifa zinazowatenganisha.

STAA wa filamu nchini, Riyama Ally, ameibuka na kauli kuhusu taarifa za kutengana na mume wake, Leo Mysterio, baada ya Mwanaspoti kuwanasa hivi karibuni wakiwa pamoja.

Riyama na Mysterio walifunga ndoa Juni 16, 2016 na Juni 2026 wakatimiza miaka 10 ya ndoa yao, licha ya mara kadhaa kuibuka kwa taarifa zinazowatenganisha.

Akizungumza na Mwanaspoti, Riyama amesema watu wamekuwa na tabia ya kuzungumza kuhusu maisha yao bila kuwa na uhakika, lakini yeye haoni sababu ya kuingia kwenye mabishano.

RIYAM 01

“Watu wakiamua kusema lao wanasema bila kuwa na uhakika wa jambo, hivyo wakiwa wanasema mimi huwa naangalia tu, kwani sina muda wa kujibizana nao kuhusu maisha ya ndoa yangu,” amesema Riyama.

RIYAM 02

Kauli hiyo imekuja baada ya kuonekana tena akiwa na Mysterio, huku ikifuatia taarifa zilizowahi kusambaa kwamba wawili hao wameachana.

RIYAM 03

Riyama, ambaye amekuwa kwenye ndoa hiyo kwa miaka 10, anaonekana kuchagua kuwaacha watu waendelee kusema yao huku yeye akiendelea na maisha yake bila kujibu kila kinachozungumzwa kuhusu ndoa yake.