Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Riyama anarudi upyaa na Huba

RIYAMA Pict

Muktasari:

  • Riyama amesema tamthilia hiyo ya muda mrefu ina waigizaji wengi bora na anatambua hilo, lakini haimnyimi nafasi ya kufanya vizuri na kurudi kwenye ushindani.

SIKU chache tu tangu alipofichua yupo mbioni kurudi katika sanaa ya uigizaji baada ya kusimama kwa muda, mwanadada Riyama Ally anajiandaa kuonekana katika tamthilia ya Huba.

Akizungumza na Mwanaspoti, Riyama amesema; “Nilikwambia mapema kiti changu kipo wazi katika sanaa, sasa nimerudi Huba ni sehemu ya mwanzo tu, mambo mengi yanakuja, hii ni kazi niliyochagua na nimezaliwa na kipaji, mashabiki zangu watarajie ubora.”

“Huba ni chaguo sahihi, nimetua katika tamthilia bora ambayo inafanya vizuri, hawajafanya makosa kunipa nafasi, nitakuwa bora. Hii nafasi itanirudisha sokoni kwa kishindo,” aliongeza mwanadada huyo aliyeanza kutamba na maigizo miaka ya 2000 akiwa na makundi ya Taswira, Tamba Arts na White Elephant.

Riyama amesema tamthilia hiyo ya muda mrefu ina waigizaji wengi bora na anatambua hilo, lakini haimnyimi nafasi ya kufanya vizuri na kurudi kwenye ushindani.

“Filamu haina darasa ni kusoma vizuri mwongozo ‘script’ na kuifanya kwa uhalisia ili kufikisha ujumbe kama inavyotakiwa tofauti na wale wanaokaririshwa mambo. Huwezi kuwa mwigizaji unameza maneno, sijisifu, lakini mimi naigiza uhalisia na nafikisha ujumbe inavyotakiwa.”