Rayvanny afanya kweli
MWANAMUZIKI, Rayvanny amekonga nyoyo za mashabiki juzi jioni wakati akizindua kampeni ya Vuna Deile inayofanyika kote nchini ikilenga kutoa zawadi mbalimbali kwa Watanzania kipindi hiki cha Sikukuu za mwisho wa mwaka na mwakani.
Miongoni mwa zawadi hizo ni pesa taslimu Sh10 milioni na gari moja mpya aina ya IST kila siku kuanzia leo.
Akizungumza katika shoo ya kutambulisha kampeni hiyo, mwanamuziki huyo ambaye jina lake halisi ni
Raymond Shaban Mwakyusa alisema huo ni mwanzo wa kufanya vitu vingine vingi vizuri.
"Leo ilikuwa ni shoo ya kutambulisha kampeni hii, mashabiki wangu na Wananchi wakae mkao wa kula, mambo mengi mazuri yanakuja katika kampeni hii ya Vuna Deile," alisema Rayvanny.
Katika shoo yake, iliyofanyika kwenye viwanja vya ITV, Rayvanny aliimba nyimbo kadhaa zilizokonga nyoyo za mashabiki kama ule wa Forever, Nakupenda na nyingine nyingi.
"Kama nilivyosema mambo mazuri yanakuja kwenye Vuna Deile, mashabiki na Watanzania wajiandae, wapo watakaoshinda ndinga, wengine mkwanja kila siku," alisema.
Akizungumzia kampeni hiyo, Naseem Allan ambaye ni mratibu alisema inatoa nafasi kwa kila Mtanzania kucheza.
"Kipindi hiki cha Sikukuu za mwisho wa mwaka na hata mwakani mambo yatakuwa ni mazuri kwa wachezaji wetu, tumetoa fursa hii ili kuwapa mzuka wa kusherehekea Sikukuu vema wakiwa na pesa na wengine kushinda magari," alisema.
Alisema kuanzia leo Jumatano, washindi 10, kila mmoja ataondoka na kitita cha Sh1 milioni.
"Pia kuna zawadi ya gari IST mpya kila siku kwa mshindi mmoja, hii inakuwa imelipiwa kila kitu, unachohitaji ni leseni tu ili kuanza kuiendesha," alisema Naseem na kufafanua kwamba kampeni hiyo ni endelevu hadi mwakani na kila siku inatoa washindi 10 wa milioni moja kila mmoja, na mshindi mmoja wa gari.
"Leo tumezindua kampeni hii ambayo unacheza kwa buku (Sh1000) na kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kushinda," alisema.
Alisema kampeni hiyi inafanywa kwa ushirikiano na ITV ambako itaonyeshwa mubashara kila siku kuanzia saa 12 jioni.
"Zawadi ni nyingi na kila Mtanzania anaweza kucheza kwa kuzingatia vigezo na masharti, itafanyika kila siku na hii inaonyesha ni namba gani tunavyokwenda kuumaliza mwaka na kuanza mwingine vizuri," alisema.
"Kifupi unapanda buku, unavuna ndinga na Sh10 milioni kwa watu 10 kila siku wanagawana," alisema.
Utaongea zaidi tutakapokamilisha vitu vyote, leo ni pafomance yaa hii kampeni ila mambo mazuri yanakuja
kampeni hiyo yenye kauli mbiu ya panda, vuna utimize ndoto inachezwa kwa namba ya kampuni 664455 na kuweka kumbukumbu namba ambayo ni namba ya simu yako kwa Sh1000 unaingia kwenye kinyang'anyiro.