Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Profesa Jay: Kwasasa nipo imara, naendelea vizuri

Msanii wa Hip Hop nchini, Joseph Haule maarufu Profesa Jay leo Mei 2 amejitokeza kwenye akaunti yake ya Instagram akipost picha yake tangu alipofanya hivyo mwaka jana akitoa ujumbe kuwa yupo imara na anaendelea vizuri.

Ameandika; "Kwanza namshukuru sana Mungu aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai, hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu).

Pili kipekee namshukuru sana Rais Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na nje ya nchi, asante sana Mama pamoja na serikali yako yote kwani viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji.

Tatu namshukuru sana Mwenyekiti wa chama changu cha Chadema Kamanda Freeman Mbowe, wanachama na viongozi wote waandamizi wa chama kwa jitihada zao za kuhakikisha napata matibabu bora zaidi kwa kushirikiana na serikali, zaidi nawashukuru sana madaktari na manesi wote wa Muhimbili na kote nilikopitia kwa kunipa matibabu ya kiwango cha juu kwa zaidi ya mwaka mzima niliolala hapo Muhimbili hasa zile siku 127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa uwezo wenu wote kuhakikisha kuwa mnaokoa uhai wangu.
Mwisho na kwa umuhimu mkubwa sana nawashukuru sana Watanzania wote mliojitolea kwa maombi na michango ya fedha zenu kuhakikisha natibiwa na kusema ukweli ilinisaidia sana kulipa bills za awali kabla ya serikali kuamua kuingilia kati na kuubeba mzigo huu asanteni sana na sitowasahau,"

Profesa Jay aliyezaliwa mwaka 1975 anakumbukwa kwa albamu zake zilizotamba za Machozi Jasho Na Damu, Aluta Continua, Mapinduzi Halisi na J.O.S.E.P.H.