Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Phina, Enioluwa waunganisha mapenzi na muziki, waja na wimbo mpya

Muktasari:

  • Sarah Michael ‘Phina’ ni msanii wa Bongo Fleva, huku Enioluwa Adeoluwa akiwa msanii wa maudhui, muigizaji na mtangazaji kutoka Nigeria.

MWANAMUZIKI wa Bongofleva, Sarah Michael Kitinga maarufu Phina na Enioluwa Prince Adeoluwa maarufu Enioluwa ni wapenzi ambao uhusiano wao umeendelea kuibua gumzo katika ulimwengu wa burudani, huku ukaribu wao ukizidi kuonekana  kupitia kazi za muziki na kuvuta hisia za mashabiki.

Sarah Michael ‘Phina’ ni msanii wa Bongo Fleva, huku Enioluwa Adeoluwa akiwa msanii wa maudhui, muigizaji na mtangazaji kutoka Nigeria.

Ukaribu wao umeendelea kuzungumziwa kutokana na namna ambavyo mapenzi yao yameunganishwa na muziki, lugha na mwingiliano wa tamaduni za Afrika Mashariki na Magharibi.

Kupitia ukurasa wa instagram, Eni alichapisha kionjo cha wimbo wake mpya  anataotarajia kutoa usiku wa leo ‘kilakshar’ ambao ameshirikiana na mpenzi wake Phina na umetumia  lugha ya kiswahili.

Jambo linaloonyesha namna Eni anavyozidi kuizoea lugha hiyo kupitia ukaribu wake na Phina, huku ushirikiano wao ukiendelea kuunganisha mapenzi na muziki katika kuvutia mashabiki wa pande zote mbili kutoka Tanznaia na Nigeria.

Hata hivyo, hii siyo mara ya kwanza kwa Phina na Eni kushirikishana katika muziki, kwani tayari wamewahi kutoa nyimbo nyingine tatu zikiwemo Smile for Me uliotoka Agosti 31, 2025, ‘Nakwamini’ uliotoka Februari 14, 2026 pamoja na ‘I Do’ iliyotoka Aprili 22, 2026.

Phina ameendelea kujijenga na kuwa msanii mwenye nafasi yake katika Bongo Fleva, huku shughuli zake za kimuziki zikiendelea kuzungumziwa sambamba na maisha yake binafsi.

Baadhi ya mashabiki wanaona uwepo wa Eni katika maisha yake umeongeza hamasa na kuleta mazingira mapya ya kihisia.

Ikumbukwe kuwa mwanzo wa kufahamiana kwa Phina na Enioluwa unahusishwa na harusi ya Jux na Priscilla Ojo, ambaye ni rafiki wa karibu wa Enioluwa na kupitia tukio hilo, Eni alipata nafasi ya kufahamiana na Phina, na ukaribu wao ukaendelea kukua hadi kuwa uhusiano wa kimapenzi.

Urafiki huo umegeuka kuwa safari inayowaunganisha katika maisha binafsi na kazi za muziki, huku ushirikiano wao ukiendelea kuvutia hisia za mashabiki wa Tanzania na Nigeria.