Ommy Dimpoz: Utanashati wangu unaniponza
Muktasari:
- Taarifa hiyo iliyotolewa leo, Septemba 18, 2026 imeeleza kuwa Wizara haikushirikishwa katika mchakato huo, hivyo haitambui jezi hizo ambazo siku chache zilizopita zilitangazwa na naibu wake, Hamis Mohamed Mwinjuma 'Mwana FA'.
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amesema utanashati wake na aina ya picha anazoweka kwenye mitandao ya kijamii ni miongoni mwa vitu vinavyomponza, kwa kuwa humletea maoni mengi, yakiwamo mazuri na ya kumshambulia.
Dimpoz ni miongoni mwa wasanii wanaopenda kuonekana nadhifu na amekuwa akiposti katika mitandao ya kijamii na mashabiki kutoa maoni tofauti kuhusu mwonekano wake
Akizungumza na Mwanaspoti, Dimpoz baada ya kuulizwa kuhusu picha zake kushambuliwa pindi anapoziposti, amesema kinachomponza zaidi ni utanashati wake pamoja na picha anazoweka, hali inayomfanya apokee maoni mengi kutoka kwa watu.
“Kinachonigharimu ni utanashati wangu na post zangu, ndiyo maana napata maoni mengi na mengine ni mabaya,” amesema Dimpoz.
Pamoja na maoni hayo, Dimpoz ameendelea kutumia mitandao yake kushirikisha mashabiki picha, taarifa za kazi zake na matukio mbalimbali yanayohusu maisha yake ya kisanii.