Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Twanga Pepeta, Nyoshi, christian Bella kuiteka Mwanza

TWANGA Pict

Muktasari:

  • Majina yanayotajwa kukutana jijini huko ni Nyoshi El Saadat na Christian Bella pamoja na msanii Phina watakaokiwasha kupamba uzinduzi huo ambao ni wa pili baada ya awali kufanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Agosti 7, 2026.

MAJINA makubwa katika muziki wa dansi yanatarajiwa kufanya shoo ya kihistoria jijini Mwanza, kwenye Ukumbi wa The Climax, Rock City Mall kusindikiza uzinduzi wa albamu ya Twanga Pepeta ya Ça Va Bien ambayo ni ya 16 kwa bendi hiyo maarufu nchini.

Majina yanayotajwa kukutana jijini huko ni Nyoshi El Saadat na Christian Bella pamoja na msanii Phina watakaokiwasha kupamba uzinduzi huo ambao ni wa pili baada ya awali kufanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Agosti 7, 2026.


TWA 01

ILIVYONOGA MLIMANI CITY

Katika shoo hiyo ya Mlimani City, bendi hiyo ambayo imekuwa tishio nchini kutokana na historia yao, ilipiga nyimbo mpya za albamu hiyo zikiwamo Ça Va Bien, Dear X, Usikariri na Usinitoe Roho, kabla ya kurudi kwenye hazina yao ya zamani iliyowahi kuwatengenezea jina kwa nyimbo kama Password, Mwana Dar es Salaam, Walimwengu, Mmbeya, Mtu Pesa, Saudia Injinia, Aminata na Sumu ya Mapenzi, huku hali ya ukumbi ikibadilika kwa mashabiki kuonyesha ushirikiabno wakicheza sambamba na bendi hiyo.


TWA 03

MAPYA YANATUA MWANZA

Twanga Pepeta Ça Va Bien Live Experience imegeukia Mwanza na ladha mpya inatarajiwa kutokana na uwepo wa nyota wengine wakiwamo Nyoshi na Bella ambao wanatarajiwa kupiga shoo ya maana.

Kwa Nyoshi amekuwa sehemu ya kizazi cha wanamuziki waliotoa mchango mkubwa katika kuufanya muziki wa bendi kuwa na ushindani mkubwa katika miaka mbalimbali.

Ndiye aliyeinyanyua FM Academia na Bogos Musica, hivyo inatarajiwa atafanya makubwa, sawa na Bella ambaye sauti yake na nyimbo zake zimekuwa zikitikisa anga ya muziki wa dansi nchini.


TWA 02

ÇA VA BIEN IMELETA MAKUBWA

Pamoja na uzinduzi wa albamu hiyo, Twanga Pepeta emepata neema ya kupokea seti ya mpya ya vyombo vya muziki vyenye gharama ya zaidi ya Sh100 milioni, huku kiongozi wa bendi hiyo Charz Baba akieleza kuwa mpango ulikuwa kuanza kuvitumia katika uzinduzi wa albamu.

Pia, kabla ya uzinduzi, bendi hiyo ilizindua studio yake mpya Magomeni Usalama, Dar es Salaam, hatua iliyotajwa kuwa sehemu ya mpango mpana wa kuimarisha shughuli zake za muziki na ndiyo maana Ça Va Bien inaenda kuisimamisha Mwanza kwa burudani tamu.