Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harmonize: Hata bila ustaa, ningewakamata tu!

Hermonize Pict

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Harmonize amesema kujiweka vyema kimuonekano mzuri sio kwa lengo la kupata warembo tu, ila ni kwa sababu ya kazi na ustaa na kwamba hata asingekuwa staa bado anaamini angekamatia wengi tu.

Akizungumza na Mwanaspoti juu ya muonekano alionao, Harmonize aliyeshirikishwa katika ngoma mpya ya ‘Simuoni’ na mkongwe wa Bongo Fleva, Ambwene Yessayah  ‘AY’, alisema; “Ukishakuwa msanii lazima uwe na muonekano utakaomvutia kila mtu, usiangalie tu mwanamke, unajua kuna muda hata bosi mwenye kampuni au mwenye matangazo anaweza akavutiwa hata na mwili wako ili kufanya nawe tangazo, hivyo ukiwa msanii ni vizuri ukatengeneza mwili wako uwe bora zaidi.”

Harmonize alisema hata kama asingekuwa msanii au staa bado angepata watoto wazuri kutokana na muonekano wake, ila hicho sio kitu cha msingi sana kwa sababu hajakipa kipaumbele kwenye maisha yake huwa anawaza kazi mapenzi baadaye.

“Tatizo watu hawanifahamu vizuri, wanadhani mimi mapenzi yamenielemea tofauti na kazi, mimi siko hivyo dadaa.. Huwa nawaacha watu waseme wanachokidhani, na kutoa nyimbo kila wakati hii ni sababu ya kupenda kazi na sio kama wasemavyo eti nikitibuana na mpenzi ndo natoa kazi kali,” alisema.