Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muziki umewakutanisha kisha ukawapa watoto

Muktasari:

  • Ndani ya Bongofleva kuna wasanii walikuwa wapenzi na pengine hadi sasa wapo pamoja, wakafanya muziki pamoja na baada ya muda wakajaliwa watoto ambao wakikua watasema hizi ni kolabo za wazazi wetu. 

Kwa kipindi chote mashabiki wanawaona kama wanamuziki waliopendana kisha wakafanya kazi pamoja lakini kuna watu wanawatazama kama Baba na Mama wameamua kufanya muziki pamoja.


Ndani ya Bongofleva kuna wasanii walikuwa wapenzi na pengine hadi sasa wapo pamoja, wakafanya muziki pamoja na baada ya muda wakajaliwa watoto ambao wakikua watasema hizi ni kolabo za wazazi wetu. 


1. Nahreel na Aika (Navy Kenzo)

Kundi hili liliundwa mwaka 2013 mara baada ya kuvunjika kwa kundi la Pah One, hata hivyo Nahreeh na Aika walikuwa wamenza muziki tangu mwaka 2008 wakati wanasoma India (Punjab College) ambapo mapenzi yao yalianzia pia. 


Mwaka 2014 Nahreel alifungua studio yake 'The Industry' baada ya kufanya kazi kwenye studio kadhaa kama Kama Kawa Records chini ya  G-Solo na Switch Records yake Quick Rocka.
Navy Kenzo ambao wameachia ngoma kali kama Kamatia Chini, Game, Fella, Katika, Why Now, Bajaj, Morning, Feel Good, Magical, Manzese, Company n.k, tayari amejaliwa watoto wawili wa kiume ambao ni Gold (2017) na Jamaica (2019).

 
Hadi sasa Navy Kenzo wamefanikiwa kutoa albamu tatu, AIM (Above Inna Minute) (2016), Story Of The African Mob (2020) na Most People Want This (2023), huku akishinda tuzo za TMA, Soundcity MVP, EATV Awards, Hipipo, WatsUp Awards na kadhalika. 


2. Ruby na Kusah

Inafahamika kuwa Ruby ni mwimbaji mzuri wa studio na jukwaani, huku Kusah  akiwa ni ni mwandishi mzuri wa nyimbo na ameshawaandikia wasanii kadhaa Bongo na nyimbo zao kufanya vizuri.


Hivyo kukutana kwao katika uhusiano ulikuwa ni mwanzo mwingine wa kuinuana kimuziki, Kusah ameandika wimbo wa Ruby 'Ntade' ambao ulifanya vizuri sana na kumrudisha katika muziki baadae ya ukimya mrefu.


Kwa kipindi walichokuwa wote walifanikiwa kutoa nyimbo tatu ambazo ni 'Kelele', 'Chelewa' na 'Nandondosha'. Baada ya nyimbo hizo ukawa mwisho wa penzi lao wakiwa tayari wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kike aliyezaliwa mwaka 2019. 

3. Izzo Bizness na Abela Music (The Amazing)

Rapa Izzo Bizness na Abela Music waliunda kundi lijulikanalo kama 'The Amazing' katikati ya mwaka 2016, Abela ni muimbaji aliyekuwa na makazi yake nchini Marekani mwenye asili ya Bukoba, Tanzania.


Mara baada ya kuunda kundi wimbo wao wa kwanza kutoa unaitwa 'Dangerous Boy' uliotayarishwa na prodyuza Dupy, huku video ikiongozwa na Focus Films chini ya Director, Nick Dizzo. Baada ya hapo waliweza kutoa nyimbo nyingine zilizofanya vizuri kama Umeniweza, Tumeoana na Rafiki.


Kipindi wakifanya kazi hizo walikuwa wakitupilia mbali tetesi za kuwa na uhusiano wa kimapenzi, hata hivyo mara baada ya Abela kujifungua watoto pacha hapo Aprili, 2018 akiwa Marekani ndipo ukapatikana uthibitisho kuwa wawili hao walikuwa pamoja penzi.