Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muziki katika ulimwengu wa tiba

Muktasari:

  • Ushahidi huo umejumuishwa katika mapitio ya Shirika la Afya Duniani (WHO) yaliyofanya tathmini ya zaidi ya tafiti 3,000 kuhusu mchango wa sanaa katika afya na ustawi wa binadamu.

Muziki ambao mara nyingi huhusishwa na burudani, starehe na sherehe, sasa unaendelea kupewa nafasi katika mjadala wa afya kutokana na tafiti zinazoonyesha kuwa unaweza kusaidia kupunguza wasiwasi, maumivu na msongo wa mawazo kwa baadhi ya wagonjwa.

Ushahidi huo umejumuishwa katika mapitio ya Shirika la Afya Duniani (WHO) yaliyofanya tathmini ya zaidi ya tafiti 3,000 kuhusu mchango wa sanaa katika afya na ustawi wa binadamu.

WHO ilisema ushahidi unaonyesha sanaa inaweza kuwa na nafasi katika kuzuia baadhi ya matatizo ya afya, kukuza ustawi na kusaidia katika usimamizi na matibabu ya baadhi ya magonjwa.

Utafiti wa mwaka 2025, uliochapishwa katika BMC Psychology, uliangalia tafiti tisa za majaribio zilizohusisha wagonjwa 787 wenye maumivu ya muda mrefu. Watafiti walibaini kuwa tiba ya muziki ilihusishwa na kupungua kwa maumivu na dalili za huzuni, ingawa hawakupata ushahidi wa kutosha kuonyesha maboresho katika wasiwasi na ubora wa maisha.

Kwa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji, mapitio ya tafiti 30 za majaribio yaliyohusisha watu 2,280 yaliripoti kupungua kwa wasiwasi, maumivu, shinikizo la damu na mapigo ya moyo kwa waliopokea uingiliaji wa muziki ikilinganishwa na huduma ya kawaida.

Akizungumza kuhusu muziki unavyotumika kama sehemu ndogo ya tiba kwa baadhi ya wagonjwa, Daktari Bingwa wa Tiba kwa Njia ya Vitendo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aisha Siraji, amesema sanaa hiyo inatumika kuwasaidia wagonjwa wanaopata changamoto ya kudhibiti hisia zao pamoja na wale wenye maumivu makali.

Amesema unatumika muziki laini kwa baadhi ya wagonjwa wenye changamoto za afya ya akili, maumivu makali na watoto wenye changamoto kama usonji, kwa lengo la kuwasaidia kudhibiti hisia na kubadili mtazamo wao kuhusu maumivu.

“Wagonjwa wenye maumivu makali kama wanaofanya dialysis au wenye saratani, ambao mara nyingi wanakuwa na maumivu, wakati mwingine tunatumia muziki ili kuwabadilisha mawazo waweze kufikiria vitu vingine.

“Tunawaweka kwenye eneo lililotulia sana, tunafungulia muziki laini sana. Hatuwezi kuweka singeli au Bongo Fleva,” amesema.

Amesema wagonjwa wanaoshindwa kudhibiti hisia mara nyingi muziki hutumika kama sehemu ndogo ya matibabu yao, pamoja na njia nyingine za tiba.

“Muziki unasikilizwa kwa saa moja na matokeo si ya siku moja. Matokeo yanapatikana ndani ya vikao kuanzia vinne na inategemea na mgonjwa mwenyewe,” amesema.

Kwa mujibu wa watafiti, matumizi ya muziki katika afya yanaweza kuonekana zaidi kama nyongeza ya matibabu badala ya kuchukua nafasi ya dawa au huduma nyingine za kitabibu. Matokeo yanaweza kutofautiana kulingana na aina ya ugonjwa, mazingira ya matibabu, aina ya muziki na namna unavyotumika.

Akizungumza na Mwananchi, mtayarishaji wa muziki nchini kutoka Mv09 Records, Ommy Dady Tz, anasema muziki ni tiba kwa sababu hubadilisha hisia za mtu, akitolea mfano mawazo.

Anasema wapo wasikilizaji wanaosikiliza kama tiba, vilevile wasanii wanaoimba kama tiba kutokana na kile wanachopitia.

“Upo umuhimu wa wazalishaji muziki kushirikiana na madaktari na wataalamu kwa sababu wazalishaji ndiyo wanaojua aina ya muziki,” amesema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dk. Herbert Makoye, anakubaliana na tiba inayotolewa na muziki, akisema sanaa hiyo inaweza kutumika kuondoa mawazo na kurudisha kumbukumbu.

“Muziki unaenda kwenye akili moja kwa moja ndiyo maana hata watoto wanaimbiwa ili walale. Aina au maneno ya muziki husika unaweza kumfanya msikilizaji kupata tiba, mfano mtu mwenye maumivu makali anaweza kupata auheni,” anasema.

Anasisitiza umuhimu wa kuungana kati ya watayarishaji na madaktaritari