Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muvi ya wiki One Night In Bangkok

MUVI Pict

Muktasari:

  • Picha linaanza kwa Kai akiwasili Bangkok kisha kukodi teksi kwa usiku mzima. Anamchagua dereva wa kike aitwaye Fah bila ya mwanadada huyo kujua abiria wake amekuja na dhamira ya kuua tu.

KAI Kahale nafasi iliyoigizwa na mkongwe wa filamu za mapigano, Mark Dacascos, mtu mwenye sura ya upole na utulivu aliyeibuka Bangkok, Thailand akiwa na siri nzito kifuani iliyojaa chuki ya kisasi kwa wabaya wake.

Picha linaanza kwa Kai akiwasili Bangkok kisha kukodi teksi kwa usiku mzima. Anamchagua dereva wa kike aitwaye Fah bila ya mwanadada huyo kujua abiria wake amekuja na dhamira ya kuua tu.

Kadri usiku unavyoendelea, Kai anamuelekeza Fah ampeleke katika maeneo mbalimbali ya jiji na kila kituo kinafichua upande wa giza wa dhamira aliyonayo, kwani jamaa anatekeleza mauaji yaliyopangwa dhidi ya watu aliowahusisha na kifo cha familia yake miaka iliyopita.

Mauaji haya yanafanywa kwa ustadi mkubwa, yakimuonyesha Kai kama mtu aliyefunzwa kivita na asiye na hofu.

Polisi wanashtuka na kuanza kufuatilia mauaji yanayoliweka jiji la Bangkok katika hali tete, hasa baada ya kugundua mtiririko wa mauaji yanayofanana na msako unaanza kumkaribia Kai.

Mwanadada Fah naye anaanza kugundua ukweli wa safari hiyo ya ajabu na kutambua, amekuwa sehemu ya mpango wa hatari bila hiari, kwani ghafla anageuka shahidi wa safari isiyo ya kawaida. Humo ndani mikono inatembezwa sana kibabe, silaha zinapigwa na kuna unyama mwingi, hadi pale Polisi wanapofanikiwa kumuua Kai, lakini akiwa amekamilisha kisasi chake, akimuacha Fah akiwa hai, lakini aliyeathirika kisaikolojia na matukio yote ya usiku huo mmoja jijini Bangkok.

Filamu hiyo imetengenezwa mwaka 2019 na kutoka 2020 ikiongozwa na Wych Kaosayananda ‘Kaos’, ikiwa na muda wa dakika 105, ikiigizwa na Mark Dacascos, Vanida Golten, Prinya Intachai, Sahajak Boonthanakit, Charlie Ruedpokanon na Michael S. New. Tukutane Ijumaa ijayo.