Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MUSIC FACTS: Professor Jay alimtosa Suma Lee na kumchukua Ferooz

NYIMBO zake zimefanya mapinduzi na kuondoa dhana kuwa muziki ni uhuni, ni miongoni mwa wasanii wakongwe wa Bongofleva wenye albamu nyingi baada ya Sugu, Lady Jaydee na Soggy Doggy.
Ameshinda tuzo za muziki Tazania (TMA), BBC n.k, huku akitoa albamu nne, Machozi Jasho na Damu (2001), Mapinduzi Halisi (2003), J.O.S.E.P.H (2006) na Aluta Continua (2007). Huyu ndiye Professor Jay;

1. John Dilinga maarufu kama DJ JD ndiye aliyempa Professor Jay jina hilo, kabla ya hapo msanii huyo alijulikana kama Nigga J, na katika moja ya shoo za DJ JD ndipo Professor Jay alimuona Jay Moe kwa mara ya kwanza na kumshirikisha katika wimbo wake, Tathmini.

2. Professor Jay sio miongoni mwa waanzilishi wa kundi la Hard Blasters Crew (HBC) kama wengi wanavyodhani, alikuta kundi tayari lipo na akajiunga nalo mwaka 1995, wakati huo Jay alikuwa kidato cha tano.
Hata hivyo, Jay aliwakuta wasanii wawili tu ndani ya Hard Blasters ambao ni Fanani na Big Willy, wanzilishi wengine wa kundi ambao ni Frank Korassa, Ngida na Taff Jam walikuwa wameenda masomoni.

3. Albamu ya kwanza ya Hard Blasters, Funga Kazi (2000) yote alifanya Prodyuza mmoja, Professor Ludigo ila 'vocals' walirekodi MJ Records, na midundo yote Professor Ludigo alikuja nayo nchini akitokea Marekani.

4. Professor Jay ameandika nyimbo tano katika albamu ya 'Funga Kazi', miongoni mwa nyimbo hizo ni Chemsha Bongo, Mamsapu, Kubwa Kuliko na Nusu Peponi Nusu Kuzimu. Baadhi ya nyimbo hizo akawapa 'verse' wasanii wengine wa Hard Blasters ili asiwe ameimba pekee yake.
Hata hivyo, wimbo wa Chemsha Bongo ilishindikana kugawa 'verse' kutokana na ujumbe wake, hivyo ikadi Jay aimbe wote pekee yake, hilo lilipelekea Fanani na Big Willy nao waruhusiwe kuingiza nyimbo zao binafsi katika albamu ili kuleta usawa.

5. Professor Jay aliandika wimbo, Chemsha Bongo akiwa kwenye daladala kutoka Kimara kwenda Posta, wimbo huu ulipotoka na kufanya vizuri kila Prodyuza alikuwa anataka kufanya kazi naye, mmoja wapo ni P-Funk Majani.
Unaambiwa Majani akiwa na Kalapina na Hashim Dogo walimfuata Professor Jay Tanga alipokuwa anafanya kazi kuzungumza naye ili akarekodi Bongo Records.

6. Wakati Professor Jay anatoa albamu yake ya kwanza, Machozi Jasho na Damu (2001) ilibidi aombe ruhusu kwa wasanii wenzake wa kundi la Hard Blasters.

7. Mwana FA alitakiwa kuwepo katika albamu ya Machozi Jasho na Damu ambapo angesikika katika wimbo, Na Bado ila Majani akagoma kuingiza 'verse' ya FA kwa madai wimbo huo umeshakamilika baada ya Jay na Imamu Abbas kurekodi.
Kipindi hicho bado Mwana FA hajatoka na Jay yupo Tanga kikazi hivyo alimtuma tu kwa Majani, ila 'verse' hiyo FA alikuja kuiweka kwenye ngoma, Hii Leo ambayo ilirekodiwa na MJ Records na Master J.

8. Profesa Jay ndiye msanii wa kwanza mkubwa Bongo kumtaja (kumrusha) Fid Q kwenye wimbo, ni katika wimbo wake, Yataka Moyo ambao unapatikana kwenye albamu yake, Machozi Jasho na Damu, hilo lilimpa sana moyo Fid Q kutafuta nafasi ya kutoka kimuziki.
Na Bwana Misosi ndiye msanii wa kwanza kuwa 'backup artist' wa Professor Jay, ndipo wakafuata wengine kama DJ Choka na Chid Benzi.

9. 'Verse' aliyochana Professor Jay katika wimbo wa Stamina, Baba (2021) aliirekodi katika studio yake, Mwanalizombe iliyopo Mikumi, Morogoro, wimbo huo ulifanya vizuri hadi Hayati Rais John Magufuli aliupenda.

10. Wimbo wa Professor Jay, Nikusaidieje (2005) tayari 'chorus' alikuwa amesharekodi Suma Lee ila baadaye wakashauriana na Majani wamuweke Ferooz kutokana alikuwa anafanya vizuri, hivyo Ferooz akakaja na kurekodi 'chorus' nyingine ambayo ndio hiyo inaisikia.
Ulikuwa ni wimbo wa pili kuachiwa kutoka katika albamu yake ya tatu, J.O.S.E.P.H (2006), video yake ilifanyika chini ya Benchmark Production, kampuni yake Madam Rita ambayo pia ndio ilifanya video ya wimbo wa Ferooz, Starehe (2004) kwa gharama ya Sh1 milioni.