Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwanini birthday ya Ja Rule ni kila baada ya miaka minne?

JA RULE Pict

Muktasari:

  • Ja Rule, mkali wa kibao cha Always On Time (2001) akishirikiana na Ashanti, alizaliwa Februari 29, tarehe ambayo katika kalenda tunayotumia wengi hujirudia kila baada ya miaka minne, na kwa miaka inayogawanyika kwa 100.

Msanii maarufu wa Hip Hop duniani, Ja Rule, mapema mwaka huu alitimiza umri wa miaka 50, lakini hakusherehekea birthday yake katika siku yenyewe kwa sababu tarehe yake ya kuzaliwa inamlazimu kufanya hivyo kila baada ya miaka minne tu.

Ja Rule, mkali wa kibao cha Always On Time (2001) akishirikiana na Ashanti, alizaliwa Februari 29, tarehe ambayo katika kalenda tunayotumia wengi hujirudia kila baada ya miaka minne, na kwa miaka inayogawanyika kwa 100.

Hadi sasa Ja Rule katika maisha yake amesherehekea birthday yake katika tarehe yenyewe, yaani Februari 29 mara 12 pekee akifanya hivyo mwaka 1980, 1984, 1988, 1992, 1996, 2000, 2004, 2008, 2012, 2016, 2020 na 2024.

Kwa mtiririko huo wa miaka, hiyo ina maana kuja kuipata tena Februari 29 katika kalenda ni hadi mwaka 2028, na hapo ndipo Ja Rule atasherehekea tena birthday yake katika siku yenyewe ambapo itakuwa ni mara ya 13 kufanya hivyo.

JA 01

Februari 29, 2016, Ja Rule alitimiza umri wa miaka 40, katika sherehe yake ya birthday alitania akisema ametimiza umri wa miaka 10 kwa sababu hiyo ndio mara ya 10 kusherehekea siku yake ya kuzaliwa katika tarehe kamili tangu kuzaliwa kwake.

Alifanya party kubwa huko Las Vegas katika night club ya Foxtail ili kuhakikisha anaweka kumbukumbu ya siku hiyo kwa sababu ni kitu ambacho kinatokea katika maisha yake kila baada ya miaka minne.

Hata hivyo, jambo la kushangaza kuhusu Ja Rule, ni kwamba alilelewa katika familia ya waumini wa Mashahidi wa Yehova, hivyo hakuruhusiwa kusherehekea siku za kuzaliwa alipokuwa mtoto ila baadaye alihama dhehebu hilo pamoja na mama yake.

JA 02

Akizungumza katika mahojiano na NBC kupitia kipindi cha Today kilichoruka Februari mwaka huu, Ja Rule amesema kuwa zamani alikuwa akipata shida kuamua iwapo asherehekee Februari 28 au Machi Mosi kama hakuna mwaka mrefu (Leap Year) ambao ndio huwa una Februari 29.

Ja Rule, mzaliwa wa New York City, amesema alijaribu kutumia tarehe hizo mbili kama mbadala wa Februari 29 lakini mwisho wa siku akaja kuamua atasherehekea birthday yake siku yoyote!.

“Kwa hiyo nilianza kufanya kitu kipya, kwa sababu nilichoka kujaribu kuamua kama nitasherehekea Februari 28 au Machi 1, kwa sababu zamani nilikuwa nafanya hivyo. Hivyo nilichoanza kufanya ni kusema kwamba sina siku maalum ya kuzaliwa.

JA 03

"Haijalishi ni lini nitaisherehekea. Nachagua siku yoyote ninayotaka, halafu tunasherehekea siku hiyo. Mwaka huu (2026) nitafanya hivyo kipindi fulani cha mwezi Machi, hata katikati ya mwezi nitatenga siku kwa ajili ya kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa,” amesema Ja Rule.

Kama alivyosema, Ja Rule alikuja kufanya birthday yake Machi 8, ambapo alisheherekea kutimiza umri wa miaka 50. Rapa huyo wa Murder Inc., alifanya hafla hiyo Las Vegas ambapo alionekana akicheza kwa mzuka wa hali ya juu.

Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Ja Rule, aliyezaliwa Februari 29, 1976, alionekana akiwa juu ya meza akicheza na kufurahia ngoma ya kundi la Hip Hop la Pretty Ricky, On The Hotline (2007).

Baada ya kuletewa keki kubwa na nzuri kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa, Ja Rule alitoa neno huku akiwa anacheka kabla ya kuzima mishumaa iliyokuwa mbele yake akisema; Ninatamani sote tuwe matajiri.

JA 04

Mbali na Ja Rule, mastaa wengine ambao birthday zao ni Februari 29, ni pamoja na mwanamuziki Korede Bello kutokea Nigeria, pamoja na mchezaji wa Hispania, Ferran Torres ambaye msimu huu amejiunga na Paris Saint-Germain (PSG) akitokea FC Barcelona.

Ikumbukwe Ja Rule aliyezaliwa na kukulia Queens, New York City, ndoto yake ya kuwa mwanamuziki mkubwa iliiva katikati mwa miaka ya 1990 akijitambulisha kupitia mitindo ya Gangsta Rap, Pop na R&B kabla ya kusainiwa na lebo ya Murder Inc.

Aligonga sana vichwa vya habari kufuatia bifu lake na 50 Cent, moja ya vita vikali zaidi vya maneno kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Hip Hop. Moto wa bifu lao ulichochewa na nyimbo za matusi na malumbano ya hadharani.

Chanzo cha bifu lao kilihusisha mchanganyiko wa migogoro ya mitaani, wivu wa mafanikio, na masuala ya biashara ya muziki. 50 Cent ambaye bado alikuwa akijitafuta, alihisi Ja Rule na kundi lake walikuwa wanamdharau na kumzuia kupata nafasi kwenye Hip Hop ya New York.

Hata hivyo, kadiri 50 Cent alivyozidi kupata umaarufu kupitia albamu yake, Get Rich or Die Tryin’ (2003), ndivyo na uhasama wao ulizidi kuongezeka. Wakati huo huo, lebo ya Murder Inc ilianza kuyumba kutokana na matatizo ya kisheria huku 50 Cent akiendelea kuwashambulia akishirikiana na kundi lake la G-Unit.