Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

20 Percent: Simu ya Sugu ilinistua

DAKIKA Pict

Muktasari:

  • Kwa 20 Percent, haikuwa simu ya kawaida. Alikuwa anamfahamu Sugu na kumheshimu, lakini hawakuwa na mazoea ya kuwasiliana moja kwa moja. Ndiyo maana aliposikia simu ikiita, akabaki akijiuliza kulikoni.

SIMU moja tu ilibadilisha siku ya msanii Abbas Hamisi Mohamed maarufu 20 Percent, baada ya jina la mwanasiasa na mwanamuziki mkongwe, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, kuonekana kwenye simu yake.

Kwa 20 Percent, haikuwa simu ya kawaida. Alikuwa anamfahamu Sugu na kumheshimu, lakini hawakuwa na mazoea ya kuwasiliana moja kwa moja. Ndiyo maana aliposikia simu ikiita, akabaki akijiuliza kulikoni.

Kilichofuata baada ya kupokea simu hiyo ndicho kilichomfanya msanii huyo kuamini kwamba wakati wa Mungu huwa sahihi.

Sugu alimweleza kwamba anataka kumweka kwenye Bongo Flava Honors Season Four, jukwaa linalowapa heshima wasanii waliotoa mchango mkubwa katika muziki wa Tanzania.

Na sasa Oktoba 30, mwaka huu, 20 Percent anatarajiwa kutawala jukwaa la The Super Dome, Masaki, Dar es Salaam, huku akiahidi kuwapa mashabiki kitu ambacho hawajawahi kukiona kutoka kwake. Mwanaspoti ilizungumza naye kuhusu simu hiyo, heshima hiyo na kile mashabiki wanachotarajia kukiona siku hiyo.


MWANASPOTI: 20 Percent, turudi kwanza kwenye ile simu ya Sugu. Ilikuwaje?

20 PERCENT: Kwa kweli simu ya Sugu ilinistua sana. Nilipoona jina lake kwenye simu yangu likipiga, nilijiuliza sana, “Kuna nini? Ana jambo gani?”

Nilikuwa namfahamu na namheshimu, lakini hatukuwahi kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja.


MWANASPOTI: Alipokupigia alikuambia nini?

20 PERCENT: Nilipopokea alianza kuniuliza, “Vipi kijana? Inakuwaje bwana?” Baada ya salamu akaniambia, “Nataka nikuweke katika Bongo Flava Honors msimu huu, hii inayofuata.”

Hapo ndipo nilipojua kwamba safari yangu ya kwenda kwenye usiku huo wa heshima imeanza.


MWANASPOTI: Ulishawahi kumfuata Sugu ukamwambia ungependa kushiriki?

20 PERCENT: Hapana. Nilikuwa na namba yake, lakini sikuwahi kuwa na story ya kumwambia. Siwezi kumpigia mtu ni kamwambia, “Niweke kwenye show.”

Wakati wangu wa kuwekwa kwenye show ulipofika, ndiyo Mungu akaamua iwe hivyo. Wakati wa Mungu huwa sahihi.


MWANASPOTI: Heshima hii ina maana gani kwako?

20 PERCENT: Ni jambo kubwa sana kwangu. Nilijisikia faraja na furaha kwa sababu hili ni jukwaa kubwa, lakini zaidi ni honor, yaani heshima.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikiona wasanii mbalimbali wakiheshimiwa kwenye Bongo Flava Honors. Sasa zamu yangu imefika.


MWANASPOTI: Baada ya kuwa kimya kwa muda, uliporudi kwenye muziki ukaonekana na muonekano mpya. Nini kilikufanya unyoe nywele zako?

20 PERCENT: Nilikuwa nataka kuwa na muonekano mpya kwa ajili ya mashabiki wangu. Nilikuwa kimya kwa muda mrefu, hivyo nilipoamua kurudi na kutoa wimbo wangu mpya “Funguwa”, nikaona ni vizuri nije na muonekano mpya kabisa


MWANASPOTI: Mashabiki watarajie nini Oktoba 30?

20 PERCENT: Nataka niwaonyeshe watu kwa nini nimeheshi mishwa siku hiyo. Hamjawahi kuniona nikipiga live katika ule uhalisia kabisa wa masaa mawili. Pia mashabiki watapata nafasi ya kuwaona baadhi ya wasanii ambao nimewahi kufanya nao kazi. Kwa kifupi, surprise zitakuwa nyingi.


MWANASPOTI: Nyimbo zipi zitakuwa kwenye menyu?

20 PERCENT: Nitapiga nyimbo zangu zinazotambulika, zikiwamo Ya Nini Malumbano, Ningekusamehe, Maisha ya Bongo, Binti Kimanzi, Money Money na nyingine nyingi.


MWANASPOTI: Una ujumbe gani kwa mashabiki wako?

20 PERCENT: Waje kwa wingi. Hii si siku ya kawaida kwangu. Nataka waje waone 20 Percent ambaye labda hawajawahi kumuona kwenye jukwaa kwa namna hiyo. Nitawapa muziki, burudani na surprise nyingi.