Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtoto aamini P Diddy ataachiwa kabla ya X-Mass

P DIDY Pict

Muktasari:

  • P Diddy, mwenye umri wa miaka 56 anatumikia kifungo cha miezi 50 jela baada ya kupatikana na hatia kwa makosa mawili ya kusafirisha watu kwa ajili ya uasherati.

KING Combs, mtoto wa kiume wa Rapa na Mfanyabiashara maarufu duniani, Sean ‘Diddy’ Combs amesema anaamini baba yake anaweza kuachiwa mapema kutoka gerezani kabla ya msimu wa Krismasi.

P Diddy, mwenye umri wa miaka 56 anatumikia kifungo cha miezi 50 jela baada ya kupatikana na hatia kwa makosa mawili ya kusafirisha watu kwa ajili ya uasherati.

Iliripotiwa awali anatarajiwa kuachiwa Juni 4, 2028, tarehe ambayo iliahirishwa kwa wiki nne.

Hata hivyo, King mwenye umri wa miaka 27 anaamini baba yake atarejea nyumbani hivi karibuni.

King aliambia TMZ.com: “Atakuwa njiani kurudi nyumbani. Anaendelea vizuri, kila kitu kiko sawa. Atakuwa nyumbani hivi karibuni.”

Alipoulizwa iwapo huenda nguli huyo wa hip-hop akapata msamaha wa serikali ya Marekani, King alijibu: “Tutaona. Tuombee tu.”

King pia aliulizwa jinsi familia inavyojiandaa kwa msimu wa likizo bila uwepo wa P Diddy na amesema; “Angalieni tu-huenda akarudi nyumbani kabla ya hapo.”