Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msama: Ninafanya matamasha kama huduma sio biashara

Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama amesema matamasha mbalimbali ambayo amekuwa akiandaa, huyafanya kwa ajili ya kutoa huduma lakini sio kufanya biashara.

Akizungumza katika kipindi cha ‘Gosplel Celebration’ cha Wapo Redio, leo Agosi 5, 2023, Msama alisema ni kutokana na hilo, hadi leo ana zaidi ya miaka 27 anafanya shughuli hiyo.

Msama alisema watu wanapaswa kujua kuandaa mtamasha ni gharama, hivyo wanapoingia humo walijua hilo kwani walioingia kwenye shughuli hiyo kwa lengo la kufanya biashara na kupata faida lakini mwisho wa siku hushindwa kuendelea.

 “Wengi hawaamini kwamba matamasha haya Mungu ndio mtoaji, mimi nimeshuhudia na kuziona baraka za Mungu, kwani nilipoanzia maisha yangu  na hapa nilipo ni vitu viwili tofauti.

“Pia nilishaahdi kuwa Mungu nitamtumikia kwa njia ya matamasha, kwani anastahili kupewa sifa na haya matamasha ni mojawapo ya kumtukuza na wengi hawaakunielewa na ndio maana hata tamasha la mwaka huu niliamua kulifanya bure pale Leaders,” alisema Msama.

Mkurugezni huyo alisema katika  tamasha hilo alitumia zaidi ya Sh160 milioni licha ya kuwa halikuwa la kiingilio lakini baada ya kumliza ameomna mambo mbalimbali ya mafanikio yakimjia katika maisha yake.

Aliongeza kuwa anafanya huduma hiyo kwa kuwa ipo ndani ya moyo wake na kwa kuwa anampenda Mungu  kwa kuwa amekuwa akimpigania na kuinua kipato chake.

Aliwashauri wengine wanaotaka kufanya hiyo huduma kutoangalia kupata faida kwani mwisho wa siku  wanaweza kujuta  na wakati mwingine kugombana na watu.