Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mitandao kuwainua Watanzania

MTANDAO Pict

MITANDAO inatajwa kama njia ya kuwainua Watanzania hasa wanapoitumia kwa njia sahihi na wengi wao wameanza kunufaika nayo kutokana na kuuza bidhaa, kutangaza biashara, wanaonunua na kushiriki minada inayopatikana huko.

Kutokana na wengi kushiriki minada, watapata nafasi ya kushindania bidhaa zenye thamani kubwa ambazo ni gari, pikipiki, seti ya dhahabu, simu janja, televisheni pamoja na manukato ya gharama (pafyumu).

Hili limewezekana baada ya baadhi ya Watanzania kujishindia vitu mbalimbali katika mitandao hasa inayoendesha minada ikiwamo wa PIKU na kuondoka na bidhaa mbalimbali.

Baadhi ya washindi hao ni Jeniffer Ayoub aliyeshinda jokofu, mashine ya kufulia, microwave, Jiko la kisasa la umeme, seti ya vyombo vya jikoni na mashine ya kuchakata chakula (food processor).

Jenipher ambaye aliweka dau la Sh36000, amesema amefurahi kushinda zawadi hizo za mamilioni ya pesa, huku washindi wengine akiwa ni Niovita Shayo aliyeshinda saa ya kike, seti ya manukato na Michael Ezekiel aliyeondoka na simu ya mkononi.

Ofisa Uhusiano na mnada huo, Barnabas Mbunda amewapongeza washindi hao na kuwaomba Watanzania kujiunga ili kushinda zawadi mbalimbali na kubadili maisha.

Amesema bado kuna zawadi mbalimbali zikiwamo gari, televisheni, pikipiki, dhahabu, simu janja na nyinginezo na kufafanua, jukwaa la kidigitali la PIKU linajulikana kwa kuendesha minada ya kipekee na yenye ushindani wa hali ya juu.

Amesema mipango yao mikubwa ni kupanua wigo wa mnada wao ikiwamo kuwezesha washindi kupata zawadi ya kushuhudia ‘live’ mchezo wa Yanga na Simba na michezo mengine ya ligi kuu mbalimbali duniani.

Kwa upande wake Afisa mwandamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Vivian Mboya amesema mchezo huo umekidhi viwango na kuwataka Watanzania kucheza na kujaribu bahati yao.

“Nawaomba Watanzania kushiriki katika mnada wa Piku na kujishindia zawadi mbalimbali, kampuni inaendesha droo ya kwa uwazi na zawadi zinawafikia washindi,” amesema Mboya.