Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maua Sama: Nisapotini nipate ‘Diaper’ za mtoto

SAMA Pict

Muktasari:

  • Kwa kauli yake, Maua anaweka wazi kuwa anachohitaji ni mashabiki kuendelea kuunga mkono muziki wake, akiamini kupitia kazi hiyo ataweza kujiendesha na kumudu mahitaji yake pamoja na mtoto wake.

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Maua Sama, amewaomba mashabiki na wadau wa muziki kumuunga mkono katika kazi zake ili aweze kumudu mahitaji ya mtoto wake, akitaja diaper kuwa miongoni mwa vitu anavyohitaji.

Maua ametoa ombi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, akieleza kuwa anahitaji sapoti ya mashabiki ili aweze kupata mahitaji hayo, huku akitumia nafasi hiyo kutangaza wimbo wake mpya.

“Naomba mnisapoti nipate diaper za mtoto, sina kazi nyingine,” ameandika Maua katika chapisho lake.

Katika ujumbe huo, aliendelea kuwahamasisha mashabiki kusikiliza wimbo wake mpya unaoitwa Simama, aliomshirikisha mwanamuziki Rayvanny, akiwataka kuupata kupitia kiungo alichoweka kwenye wasifu wake wa Instagram.

Mwanaspoti lilimtafuta mwanamuziki huyo kwa njia ya simu kutaka kujua kama haoni kauli yake ya kuomba sapoti ya diaper za mtoto inaweza kutafsiriwa tofauti na mashabiki wake.

Akijibu hilo, Maua amesema yeye ni mwanamuziki na muziki ndiyo kazi yake, hivyo haoni sababu ya watu kushangazwa na ombi lake la kutaka mashabiki wamuunge mkono ili aweze kuendelea na maisha.

“Mimi ni mwanamuziki, sina kazi nyingine zaidi ya muziki. Kwa hiyo kusema naomba sapoti ili nipate diaper za mtoto wangu sioni kama ni jambo la kushangaza.

“Wanichukue kama nilivyo, mashabiki wanisapoti tu kazi yangu ya muziki ili niweze kuendelea kuishi,” amesema Maua.

Maua amekuwa katika ukurasa mpya wa maisha tangu alipojifungua mtoto wake wa kwanza wa kike Septemba 2, 2026, ambapo kwa mujibu wake, amejitambulisha kwa jina la mama Falsafa ikiwa na maana kwamba mtoto wake anaitwa Falsafa.

Ujio wa mtoto huyo umeongeza majukumu mapya kwa mwanamuziki huyo, ambaye sasa anaendelea na maisha ya umama sambamba na shughuli zake za muziki.

Kwa upande mwingine, wimbo wake mpya Simama aliomshirikisha Rayvanny unaonekana kuwa sehemu ya juhudi zake za kuendelea kuwasiliana na mashabiki na kutafuta sapoti kupitia kazi zake.

Kwa kauli yake, Maua anaweka wazi kuwa anachohitaji ni mashabiki kuendelea kuunga mkono muziki wake, akiamini kupitia kazi hiyo ataweza kujiendesha na kumudu mahitaji yake pamoja na mtoto wake.