Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MATESO : Mzee Small hali tete-3

Muktasari:

  • Anasema anashindwa kufika katika vituo vya matibabu na hata hajui itakuwa vipi pale atakapotakiwa kufika kliniki kwa ajili ya mazoezi na anayaomba makampuni ambayo alipata kufanya nayo kazi yamsaidie ili aanze kliniki.

MZEE Small Wangamba angali anateseka na hajapata msaada wa maana wa matibabu na sasa anaomba wahisani wajitokeze na kushughulikia matibabu yake, ndugu wamemtelekeza amebaki na mkewe na wanae wawili ambao hata hivyo nao wanahitaji msaada wa wadau. Endelea…

Small anasema akiwa na kundi hilo la Agizo alipata fursa ya kujifunza sanaa kwa undani na kushiriki katika upigaji na uchezaji wa ngoma za makabila tofauti, maigizo, kwaya na vichekesho hadi mwanzoni mwa miaka ya 1980.

Small anasema kikundi hicho ambacho kilikuwa chini ya uongozi wa Said Seif Unono ndio ambacho kiliibua kipaji chake na hata kuonwa na vikundi vingine.

Anasema mwaka 1982 alifuatwa na kuombwa kujiunga na kikundi cha sanaa cha Muungano ambacho kilikuwa kipo chini ya Norbet Chenge ofa ambayo hakuikataa.

 “Muungano walikuwa katika mchuano mkali na vikundi vingine kama vile DDC Kibisa, Reli, Ujamaa Dancing Troupe na baadaye TOT” anasema na kuongeza kuwa hapo ndipo alipojua sanaa ni nini.

Anasema Muungano walikamilika kila idara na walikuwa wakijaza watu kila onyesho na mwaka mmoja baadaye kwa mara ya kwanza alisafiri kwenda kufundisha uchezaji ngoma nchini Uingereza.

“Siku hiyo kuna watu walikuja kutoka Uingereza na wakasema wanataka wasanii ambao wataenda kuwafundisha wa kwao nchini Uingereza,” anasema.

Wageni hao kutoka nchini humo waliambiwa kama masuala ya ngoma waje Tanzania na kikundi ambacho wangeweza kuwapata wasanii wazuri ni Muungano hivyo baada ya kutumbuiza wote pamoja wageni hao walimchagua Small na msanii mwingine aliyekuwa anaitwa Martha Charles.

“Tulifanya kazi kwa wiki tatu kabla ya kurudi nchini na baadaye kwenda Uarabuni,” anasema na kuongeza kuwa baada ya hapo akahama kundi hilo na kujiunga na lile la Reli na wakati huo kulikuwa na msukumo wa michezo na sanaa makazini.

Anasema alidumu kwa muda na kundi hilo na miaka michache baadaye mambo yakaanza kwenda kombo hivyo akawa akawa anafanya kazi kivyake na wasanii wachache wakati mwingine kufa kwa makundi kukamfanya ajitose katika promosheni na kazi zingine.

“Nashukuru nimesafiri mikoa mingi nchini nikifanya maigizo na vichekesho kutoka sehemu moja hadi nyingine hadi maradhi yaliponifika hivi karibuni.”

Hali ya sasa

Small anasema anashukuru kwa misaada ya wahisani mbalimbali ambayo imemsaidia kuweza kujikimu kwa kupata lishe na huduma zingine lakini kutokana na maradhi yake yalipofikia anasema anahitaji msaada wa matibabu.

Anasema anashindwa kufika katika vituo vya matibabu na hata hajui itakuwa vipi pale atakapotakiwa kufika kliniki kwa ajili ya mazoezi na anayaomba makampuni ambayo alipata kufanya nayo kazi yamsaidie ili aanze kliniki.

Mkongwe huyo anasema makampuni ni mengi ambayo amefanya nayo kazi hivyo anawaomba viongozi wa makampuni hayo kufanya hisani ili aweze kupata matibabu yafaayo kwani hali kwake si nzuri na anaamini kuwa akiwezeshwa wanae na mke wake wataweza kumrejesha hali ya kawaida.

Anasema kuna makampuni makubwa ambayo amefanya nayo kazi hivi karibuni na mengine bado yanatumia matangazo yake hadi  sasa na ingawa anakataa kuingia kwa undani kuhusiana na mikataba yao lakini anaomba msaada akatibiwe.

“Waje tu wanipeleke popote hata India sawa maana sijui hatma yangu na jitihada za washabiki ndio ambazo zinanifanya niwepo hadi leo kwani kazi yenyewe nilisimama mwaka mzima sasa na hata wenzangu wa Bongo Movie siwaoni tena.”

Small anasema kuwa wasanii wenzake wangekuwa wanakuja kumuona kwa umoja wao wangeweza kunisaidia nikapata matibabu yanayofaa na anabainisha kuwa siku za awali walienda kumjulia hali lakini kilichowafanya wakakata mguu hajakijua hadi sasa.

Maoni ya wadau kuhusiana na hali ya Mzee Small

Ndugu mwandishi nimesikitishwa sana na habari za ugonjwa wa Mzee Small Wangamba unachangiwa na wizi wanaofanyiwa wasanii na mapromota uchwara. Ushauri wangu ajitahidi kuomba msaada kwa Rais Jakaya Kikwete ndiye pekee ndio atakayemsaidia-Shabiki wake, Dar es Salaam.

--------

Pole sana mzee wangu Small Mungu atakusaidia utapona na Ishallah. Shabiki wake Mwanza

Naitwa Hassan M Haji nipo Zanzibar umri miaka 48

kwa miaka minne nimepata matatizo kama yako wezi walitumia ugonjwa wangu kuniibia na nimeuza shamba na nyumba usikate tamaa ipo siku utapona.

Nakuangalia kwa huruma katika gazeti la Mwanaspoti pole sana ila mazoezi muhimu.

Nasoma gazeti la Mwanaspoti nipo Babati Manyara nimeona mateso ya Mzee Small, Mungu atamsaidia.

Naitwa Msham au baba Nurat, napatikana Chamazi Dovya msomaji mzuri wa Mwanaspoti sina cha kumsaidia zaidi ya dua zangu pamoja na za Watanzania  pamoja na kumshauri kwa kuwa ni muislam amke usiku wa manane na aombe dua pia kwani ibada licha ya kuwa inasaidia lakini pia kuswali ni mazoezi, Mungu atamsaidia.

Naitwa Pendo Mushi nimesoma ripoti ya Mzee Small nimeguswa sana na kilichompata namuomba aende katika maombi atapona kabisa bila malipo.

Nipo Shinyanga nimesoma makala ya Small binafsi sina cha kumpa isipokuwa namsisitizia ashiriki maombi na Mungu atamsaidia Mungu akupe ahueni Mzee Small-Shabiki Nachingwea

Pole Mzee Small na usiache kuswali na Mungu atakusaidia pia ni vema kusoma dua mara kwa mara kabla ya kufanya jambo lolote.

Nimesoma Mwanaspoti kuhusiana na ugonjwa wa Mzee Small nashauri mpelekeni kliniki ya Wakorea ipo maeneo ya Msimbazi Polisi mimi ndugu yangu alitibiwa akapona

Habari naitwa Jaxn John mwenyeji wa Masasi nimeisoma makala ya Mzee Small habari zake zimenigusa sana na msaada wangu kwake ni ushauri kuwa aonane na madaktari na ahakikishe kuwa anaonana na madaktari wa mazoezi.

Ni vizuri wadau wakachukua jukumu la kumsaidia Mzee Small badala ya kumuacha akiteseka bila matibabu Rais JK aambiwe, Wabongo wasitake sifa katika misiba tu wawe na wanajitoa kusaidia katika magonjwa na hiki ndio kipindi cha kumsaidia-Jackson David Dar es Salaam.