Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maswali sita Ashurey, Zuchu kuna nini WCB?

MASWALI Pict

Muktasari:

  • Sasa kinachoulizwa ni kweli kuna utengano? Na kama upo, nini ndo chanzo. Kila mtu anajiuliza lake, lakini hapa kuna maswali sita ambayo Mwanaspoti limeyachakata na kujifikirisha kama mashabiki wanavyojiuliza na nini kitatokea baada ya hapo.

MOJA ya mambo yaliyoibua maswali kwa mashabiki ni uhusiano wa dansa Ashurey na Zuchu, na kwa sasa wamekuwa mbalimbali tofauti na mwanzo walikuwa na ukaribu.

Wawili hao wamekuwa pamoja kwa muda mrefu na Ashurey amekuwa akishiriki matukio makubwa ya Wasafi na kuwa karibu na Zuchu, akishiriki pia katika shoo za Diamond Platnumz.

Sasa kinachoulizwa ni kweli kuna utengano? Na kama upo, nini ndo chanzo. Kila mtu anajiuliza lake, lakini hapa kuna maswali sita ambayo Mwanaspoti limeyachakata na kujifikirisha kama mashabiki wanavyojiuliza na nini kitatokea baada ya hapo.


MASWA 02

KWA NINI HAKUONEKANA WAKATI WA UJAUZITO WA ZUCHU

Julai 30, 2026, Zuchu aliweka wazi ujauzito wake katika picha za ujauzito na vipimo vya mtoto hatua iliyopokelewa kwa furaha na mashabiki pamoja na watu mbalimbali wa burudani.

Julai 31, alifanya baby shower nyumbani kwake Mbezi Beach, huku Agosti 2 akijifungua mtoto wa kike aliyempata na Diamond Platnumz.

Katika matukio hayo, mashabiki wamekuwa wakijiuliza kuhusu kutokuwepo kwake.

Alihudhuria baby shower hiyo? Je, alikwenda kumjulia hali Zuchu baada ya kujifungua? Amewahi kwenda kumuona mtoto huyo? Na kama hawajaonekana pamoja katika matukio hayo, ni nini kimebadilika katika ukaribu wao?


KUFUTA NEMBO YA WASAFI

Hatua inayozungumziwa ya kuondoa nembo au utambulisho wa Wasafi kwenye ‘bio’ yake imeongeza maswali kuhusu nafasi yake ndani ya kundi hilo.

Je, ni uamuzi wa kubadilisha utambulisho wake wa kikazi, anajiandaa kujitegemea au kuna mabadiliko katika ushirikiano wake na Wasafi?

Hili ni jambo linalohitaji ufafanuzi wake mwenyewe, kwa sababu kuondoa jina au nembo kwenye bio pekee hakutoshi kuthibitisha ameachana na taasisi hiyo.

MASWA 01

KUKOSEKANA SHOO YA MONDI UGANDA

Safari ya Diamond kimuziki Uganda mwishoni mwa Oktoba 2026 nayo ilikuwa miongoni mwa matukio yaliyovuta hisia za mashabiki.

Hata hivyo, mjadala mwingine umeibuka kuhusu kutokuonekana kwa Ashurey katika shoo hiyo, jambo lililowafanya baadhi ya mashabiki kujiuliza sababu za kutokuwepo kwake.

Kwa kuwa Ashurey amekuwa akihusishwa na maonyesho ya Diamond, kutokuwepo kwake katika safari hiyo kumeongeza maswali kuhusu nafasi yake katika kikosi cha burudani cha msanii huyo.

Je, alikuwa na majukumu mengine? Je, hakuhitajika kwenye safari hiyo au kuna mabadiliko katika timu inayosafiri na Diamond?


NYIMBO YA ZUCHU, ASHUREY HAKUWEPO

Zuchu ni miongoni mwa wasanii wanaotumia nguvu ya mitandao kutangaza kazi zake. Mfano ni wimbo wake mpya, ‘Kucheza Unaju’ aliomshirikisha DeSmile, ambao ulipata ushiriki mkubwa wa mashabiki kupitia dance challenge.

Hata hivyo, kutokuonekana kwa Ashurey akishiriki baadhi ya chalenji za nyimbo za Zuchu kumeibua swali jingine kuhusu ukaribu wao.

MASWA 03

DIAMOND, ASHUREY KWA NINI NI YEYE?

Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakijadili staili yake ya kucheza na Diamond jukwaani, huku wengine wakihoji kwa nini yeye ndiye anayeonekana kupata nafasi hiyo katika baadhi ya matukio badala ya madansa wengine.

Hapa kuna mambo mawili yanayohitaji kutofautishwa; upande wa kwanza ni kazi yake kama dansa, na upande mwingine ni tafsiri ambazo mashabiki wamekuwa wakizitoa kutokana na ukaribu unaoonekana jukwaani.

Je, ni sehemu ya maelekezo ya burudani ya Diamond au kuna sababu nyingine inayomfanya Ashurey kuonekana zaidi katika maonyesho hayo?


LILSOSO NI MMBADALA WA ASHUREY?

Inaelezwa Ashurey ndiye aliyemfundisha Lilsoso  kucheza kabla ya kumtambulisha jambo linalofanya iwe muhimu kutofautisha suala la kufundisha dansa na kuchukua nafasi ya mtu mwingine.

Kama Lilsoso  ameendelea kuonekana katika mazingira ya burudani ya Wasafi, je, ni kwa sababu ya kupanua kikosi cha madansa au kuna mabadiliko ya majukumu?

Na kama Ashurey bado ana nafasi yake, kwa nini kutokuwepo kwake kwenye baadhi ya matukio ya wasafi kumeendelea kuibua maswali?