Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maajabu ya Grammy 2026

GRAMMY Pict

Muktasari:

  • Mashabiki walikuwa na hamu ya kuona ni nani atakayeshinda na historia itavunjwa. Mwanzo Rose na Bruno Mars waliwaka jukwaani na wimbo wa ‘Apt’ na ‘I Just Might wakitoa shoo  iliyoacha alama kwa baadhi ya mashabiki wanaopenda muziki.

USIKU wa Tuzo za Grammy za 2026 uliofanyika Februari 1, mwaka huu katika Ukumbi wa Crypto.com Arena, Los Angeles, Marekani ulikuwa wa msisimko mkubwa, burudani na mambo ya fasheni na shoo za aina yake kutoka kwa wasanii wa aina mbalimbali.

Mashabiki walikuwa na hamu ya kuona ni nani atakayeshinda na historia itavunjwa. Mwanzo Rose na Bruno Mars waliwaka jukwaani na wimbo wa ‘Apt’ na ‘I Just Might wakitoa shoo  iliyoacha alama kwa baadhi ya mashabiki wanaopenda muziki.

Mwingine ni mwanamuziki, raia wa Canada, Justin Bieber aliyepafomu kwenye tuzo hizo za 68 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1959.

GRA 01

TYLA AKOSOLEWA

Baada ya mwanamuziki wa Afrika Kusini, Tyla Laura Seethal kushinda tuzo katika kipengele cha Best African Music Performance ni kama mashabiki hawajaridhika wakiamini Davido alistahili.

Tuzo hizo ambazo ni mara ya 68 kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 1959 Marekani, mwanamuziki wa Marekani, Beyonce anashikilia rekodi ya msanii anayeongoza kuwania tuzo hizo mara 99 na rekodi ya kuchukua tuzo hizo mara nyingi zaidi (35) katika miaka tofauti.

Tyla aliyeshinda kupitia wimbo wa ‘Push to Starts’ ambao ulipokelewa vyema na mashabiki alikuwa anawania tuzo hiyo na Davido kupitia wimbo wake wa ‘With You’ aliomshirikisha Omah Lay, Burnaboy ‘Love’, Ayra Starr kupitia wimbo wa ‘Gimme Dat’ aliomshirikisha Wizkid na Youssou N’Dour (Senegal) kupitia wimbo wa Éclairer le Monde.

Sasa baada ya ushindi huo ni kama mashabiki hawajaridhishwa na ushindi wa mwanadada huyo ambaye ni mara yake ya pili kuchukua Grammy, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2024 katika kipengele cha Best African Music Performance kupitia wimbo ‘Water’, akawa msanii wa Kiafrika wa kwanza kushinda kipengele hicho.

Baadhi yao wanaamini tuzo hiyo alistahili Davido kutokana na wimbo wake na Omah Lay kupenya kimataifa na kuwa moja ya zilizofanya vizuri.

Hii ni mara ya tatu nyota huyo anakosa tuzo hizo; mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2024 na Tyla (Afrika Kusini) aliiondoka na tuzo hiyo kupitia wimbo wa Wate, uliofuata, tuzo hiyo ikaenda kwa mwanadada Tems (Love Me Jeje), na mwaka huu ikienda Tyla tena.

“Wanaume tunaweza kukosoa jinsi Davido amevunjika moyo mara nyingi katika miaka hii mingi bila kupunguza utambulisho wa Kiafrika wa Tyla na muziki wake. Tyla ni mtoto wa ardhi ya Afrika kama Davido,” alisema mmoja wa shabiki.

“Tyla ameshinda lakini Davido alistahili na atabaki kwenye mioyo yetu kuwa huyu ni mshindi wetu.”

GRA 02

KENDRICK AVUNJA REKODI

Mbali na Tyla wasanii wengine walioweka rekodi ni rapa wa Marekani, Kendrick Lamar aliyeshinda tuzo tano na kuvunja rekodi ya rapa Jay Z aliyekuwa anashikiliwa ya kuwa msanii wa hiphop aliyeshinda tuzo nyingi zaidi.

Jay-Z alikuwa na rekodi ya kuwa msanii wa hip-hop aliyeshinda Grammy nyingi zaidi (26), lakini ushindi wa Kendrick Lamar umemfanya kuwa msanii wa hip-hop aliyeshinda nyingi zaidi katika historia, baada ya kushinda 27 hadi wakati huo.

Usiku huo Lamar aliondoka na tuzo ya Mtumbuizaji Bora wa Rap kupitia wimbo wa ‘Chains & Whips’ with The Clipse, Pharrell, Albamu Bora ya Rap kupitia albamu yake ya ‘GNX’, Wimbo Bora wa Rap ‘tv off’,  Wimbo ulioandaliwa vizuri kwa kutumbuizwa ‘Luther’, Wimbo bora wa kutengenezwa ‘Luther’  na wimbo bora wa mwaka ‘Luther’.

GRA 03

FILAMU ZILIZOACHA REKODI

Ushindi wa awali ulianza mapema kwenye hafla ya alasiri kabla ya matangazo makuu. Filamu tatu zilizokuwa gumzo mwaka uliopita ziliibuka na Grammys.

‘Golden’ ya KPop Demon Hunters ilishinda wimbo bora ulioandikwa kwa Vyombo vya Habari vya Taswira, Cynthia Erivo na Ariana Grande kutoka Wicked walishinda Pop Duo/Kikundi Bora kwa ‘Defying Gravity’ na Sinners ilishinda mara mbili kwa mkusanyiko bora wa Muziki wa Filamu na Albamu Bora ya Muziki wa Filamu.

Ushindi huu ulithibitisha hata filamu zilizoachwa nje ya Oscars zinaweza kutimiza mafanikio makubwa kwenye muziki.

KPop Demon Hunters walifanya historia kwa kuwa bendi ya kwanza ya K-pop kushinda Grammy.

GRA 04

MARA YA KWANZA

Kwenye upande wa washindi wa mara ya kwanza na waliowaacha watu midomo wazi, Bad Bunny alishinda Grammys tatu zisizo za Kilatini Albamu Bora ya Mwaka na Albamu Bora ya Música Urbana kwa Debí Tirar Más Fotos, pamoja na Utendaji Bora wa Muziki wa Kimataifa kwa wimbo ‘Eoo’.

The Cure walishinda Grammy mbili za kwanza kabisa na Frank Bello wa Anthrax alikua mwanachama wa kwanza wa bendi hiyo kushinda Grammy baada ya maonyesho yake ya moja kwa moja. Olivia Dean alishinda msanii mpya bora, akiweka historia kuwa mwanamke wa tisa kushinda tuzo hiyo mfululizo.

Prodyuza Jack Antonoff naye alishinda tuzo nne usiku huo, na kushirikiana na Kendrick Lamar kwenye wimbo wa ‘Luther’ ulioshinda rekodi bora ya mwaka.

Ushindi mwingine uliowaacha midomo wazi baadhi ya mashabiki ulitokea kwa Lola Young, aliyeshinda kipengele cha ‘Mtumbuizaji Bora wa pop’ kupitia wimbo wa ‘Messy’ akiwapiku wengi waliokuwa wanatarajiwa kama Justin Bieber (Daisies), Sabrina Carpenter (Manchild), Lady Gaga (Disease) na Chappell Roan (The Subway).

Bendi ya rock ya Turnstile walishinda Albamu Bora ya Rock na Utendaji Bora wa Metal, wakizipiku majina makubwa kama Deftones na Linkin Park.

Katika kipengele cha Wimbo Bora wa Mwaka, Billie Eilish alishinda kwa ‘Wildflower’, akishinda wimbo wa KPop Demon Hunters, Lady Gaga, na Sabrina Carpenter. Washindi kutoka TikTok kama Addison Rae, Alex Warren, PinkPantheress, Katseye, na Zara Larsson walipata umaarufu mkubwa na kuingia kwenye vinyang’anyiro saba kwa pamoja, lakini waliondoka bila tuzo yoyote.