Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lady Jaydee’ kutua kivingine Arusha

JD Pict

Muktasari:

  • Jide amesema hayo kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya Bongo Fleva yanayotarajiwa kufanyika Arusha Septemba 19, mwaka huu, akieleza kuwa amewaandalia wakazi wa jiji hilo mambo mazuri.

MWANAMUZIKI mkongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, amesema ujio wake jijini Arusha hautakuwa wa kushiriki maadhimisho ya miaka 30 ya Bongo Fleva pekee, bali pia anatarajia kutumia nafasi hiyo kuwaunga mkono wafanyabiashara wadogo na kuanza kutekeleza ahadi yake ya kutoa mitaji midogo midogo.

Jide amesema hayo kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya Bongo Fleva yanayotarajiwa kufanyika Arusha Septemba 19, mwaka huu, akieleza kuwa amewaandalia wakazi wa jiji hilo mambo mazuri.

Akizungumza na Mwanaspoti, Jide amesema safari yake Arusha itakuwa na mambo mbalimbali, ikiwemo kuzunguka katika masoko na kununua bidhaa kutoka kwa wafanyabiashara kama sehemu ya kuwaunga mkono.

“Nimewaandalia watu wa Arusha vitu vizuri,” amesema Jide.

J02

Mbali na hilo, Jide amesema atapata muda wa kula kuku wa Uzunguni kwa chakula cha mchana na jioni, huku akiwa na mpango wa kuuza vitabu vyake kwa mashabiki na watu atakaokutana nao.

Hata hivyo, jambo kubwa zaidi katika safari hiyo ni mpango wake wa kuanza kutimiza ahadi aliyowahi kuitoa ya kutoa mitaji midogo midogo, ambapo amesema Arusha ndiyo sehemu atakayoanzia.

Jide ni miongoni mwa wasanii wakubwa wanaoshiriki katika Tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva, wakati yeye akiwa ametimiza miaka 25 tangu aanze safari yake katika tasnia ya muziki.

J03

Katika miaka hiyo 25, Jide amejijengea nafasi kubwa katika muziki wa Tanzania kupitia nyimbo mbalimbali zilizobeba jina lake, zikiwemo Yahaya, Joto Hasira, Niambie na Nitafanya, huku akiendelea kuwa miongoni mwa wanawake walioacha alama kubwa katika historia ya Bongo Fleva.

Tofauti na wasanii wengi wanaotumia maadhimisho kama nafasi ya kukutana na mashabiki jukwaani pekee, safari hii Jide anaonekana kutaka kupeleka sehemu ya shangwe hizo kwa watu wa kawaida, hasa wafanyabiashara anaotarajia kuwakutana nao katika masoko ya Arusha.

J01

Na kama alivyosema mwenyewe, Arusha ameandaa vitu vizuri, huku sehemu ya mpango huo ikiwa ni kuanza kutimiza ahadi yake ya mitaji midogo midogo.