Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ladha za Juma Nature Nandy Festival 2026

NANDY Pict

Muktasari:

  • Tangu mwaka 2019 tamasha hilo lilipoanzishwa na muimbaji Faustina Charles Mfinanga maarufu Nandy au African Princess, huu ni msimu wake wa tano.

TAMASHA la Nandy Festival mwaka huu kwa Dar es Salaam linaenda kuwa na sura mpya, likiwa na ladha tofauti na misimu iliyopita. 

Tangu mwaka 2019 tamasha hilo lilipoanzishwa na muimbaji Faustina Charles Mfinanga maarufu Nandy au African Princess, huu ni msimu wake wa tano.

Safari ya Nandy Festival haikuwa ya moja kwa moja kila mwaka, kwani tamasha hilo liliwahi kusimama, ikiwemo mwaka 2023 wakati Nandy alipokuwa kwenye kipindi cha ujauzito na baadaye kulea mtoto wake aliyezaa na mumewe, Billnass. Hivyo, mwaka 2026 unakuwa msimu wa tano wa tamasha hilo.

Tamasha hilo mwaka huu lilianzia mkoani Shinyanga, Juni 20 kwa mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wa Nandy katika viwanja vya ShyCom. Uzinduzi huo ulienda sambamba na sherehe za miaka 10 ya Nandy katika muziki, kabla ya msafara huo kuelekea Kigoma.

Katika safari hiyo, Nandy hajawa peke yake kwani Billnass amekuwa sehemu ya maandalizi na amekuwa akimpa sapoti kubwa katika safari ya tamasha hilo kila linapohamia mkoa mwingine, uwepo wake umeonekana kuwa sehemu ya nguvu ya maandalizi.

KIZAZI KIPYA VS JUMA NATURE
Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Dar Village, Jumamosi hii Septemba 26, 2026, litawakutanisha wasanii wa kizazi kipya akiwemo D Voice, Gnako, Pipi Jojo na Click Master.

Lakini jina la Juma Nature ndilo limeongeza uzito kwenye orodha hiyo. Nature ni miongoni mwa wasanii walioweka alama kubwa katika miaka ya mwanzo ya Bongo Fleva na amekuwa akiheshimika na mashabiki wa muziki huo.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa msanii mkongwe wa aina hiyo kushiriki Nandy Festival, jambo linalofanya tamasha la mwaka huu kuwa na ladha tofauti. Pia Linah naye atashiriki kwa mara ya kwanza.

Nature atakapokutana na wasanii wa kizazi kipya kwenye jukwaa moja, mashabiki watapata picha ya safari ya Bongo Fleva, kutoka kizazi kilichopiga hatua za mwanzo hadi kizazi kinachoendelea kuandika historia yake leo.

UPEPO WA MIAKA 30 YA BONGO FLEVA
Juma Nature kuingia kwenye Nandy Festival mwaka huu kunaongeza kitu cha pekee. Ni jina la kizazi cha zamani likikutana na wasanii wanaobeba Bongo Fleva ya sasa.

Nature anakuja na historia yake, wakati D Voice, Gnako, Pipi Jojo na Click Master wakiwakilisha upande mwingine wa muziki wa kizazi kipya.

Hapo ndipo jukwaa la mwaka huu linapata mvuto wake, kwani mashabiki watapata nafasi ya kuona mitindo miwili ya Bongo Fleva ikikutana sehemu moja.

Kwa Nandy, hii ni sehemu ya sherehe za miaka 10 ya muziki wake. Kwa tamasha, ni msimu wa tano unaokuja na sura tofauti, huku Nature akiongeza ladha ya kizazi kilichotangulia.