Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa ‘Mvua ya Baraka’, ‘Gere’ yakumbukwa

MVUA Pict

Muktasari:

  • Kwa nini? Ni kwa sababu nyimbo zote mbili Mondi kaimba na wapenzi wake, yaani, Donna aliyezaa naye na Zuchu ambaye amefunga naye ndoa na wana mtoto mmoja.

HUKO mitandaoni kuna kamjadala ka kulinganisha wimbo wa Zuchu aliomshirikisha mumewe Diamond Platnumz ‘Mvua ya Baraka’ uliotoka mwaka huu 2026 na ule wa Mondi na Tanasha Donna, Gere uliotoka mwaka 2020.

Kwa nini? Ni kwa sababu nyimbo zote mbili Mondi kaimba na wapenzi wake, yaani, Donna aliyezaa naye na Zuchu ambaye amefunga naye ndoa na wana mtoto mmoja.

Hata hivyo, wakati mjadala ukiendelea huko mitandaoni, Mwanaspoti linazilinganisha nyimbo hizo kuanzia mapokezi yao  na zilivyofanya vizuri kwenye majukwaa ya muziki.

Gere ilianza kwa kasi kubwa, ikifikisha watazamaji milioni moja ndani ya saa 11, zaidi ya milioni tatu ndani ya siku tatu na milioni 4.3 ndani ya wiki moja, kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la The Citizen.

Miaka sita baadaye, Diamond na Zuchu wamekuja na Mvua Ya Baraka, wimbo wenye ujumbe wa shukrani, imani na baraka za maisha, tofauti na Gere iliyozungumzia zaidi mapenzi na changamoto za mahusiano.

Kwa mujibu wa takwimu za ChartsList, video ya Mvua Ya Baraka iliyotoka Novemba 15, 2026, ilikuwa imefikisha watazamaji milioni 2.2 kufikia Novemba 17, ikiwa na zaidi ya likes (kupendwa) 76,000.

Nguvu ya wimbo huo haijaishia Tanzania pekee, chati ya YouTube Music iliyosambazwa na Wasafi inaonyesha kazi hiyo ilishika nafasi ya kwanza katika chati za muziki Tanzania, Kenya, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Mbali na nchi hizo, Mvua Ya Baraka ilishika nafasi ya 7 Canada na Uingereza, nafasi ya 13 Ufaransa na Saudi Arabia, huku ikiwa nafasi ya 17 nchini Ujerumani.

Hii inaonyesha namna wimbo huo ulivyoanza kupata nafasi katika masoko mbalimbali nje ya Afrika Mashariki.

Katika Shazam, Mvua Ya Baraka ilishika nafasi ya pili Tanzania, ya kwanza Kenya, ya sita Zambia na Uganda, kuonyesha kazi hiyo imevuka mipaka ya soko la nyumbani.

Tofauti nyingine ni, Mvua Ya Baraka ilianza kupata mwitikio kupitia ‘audio’ kabla ya video rasmi kuachiwa, huku Gere ikijenga kasi kubwa mara tu video yake ilipotoka.

Nyimbo hiyo imepata sapoti ya wasanii wakubwa wa kimataifa kama Davido  ameisapoti nyimbo hiyo hadharani. Aliweka katika ukurasa wake wa instagram kuwa Mvua ya Baraka ndo nyimbo yake bora kwa mwaka huu.

Kwa upande wake Diamond ameendelea kuupa nguvu wimbo huo kupitia mitandao ya kijamii, akimpongeza Zuchu kwa kazi hiyo na kushiriki baadhi ya video za mashabiki waliojiunga kwenye hii chalenji ya Mvua Ya Baraka.