Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilichombeba Jux Afrima 2026

JUX Pict

Muktasari:

  • Tuzo za Afrima (AFRIMA – All Africa Music Awards), ni tuzo za muziki zinazolenga kutambua na kuenzi ubora wa wasanii wa Afrika katika nyanja mbalimbali za muziki zikiwa na kusudio la kukuza vipaji na kuunganisha muziki barani humo.

MIONGONI mwa stori zinazotamba Afrika kwa upande wa burudani ni tuzo za muziki za Afrima zilizotolewa wiki hii nchini Nigeria ikiwa ni mara ya tisa kufanyika.

Tuzo za Afrima (AFRIMA – All Africa Music Awards), ni tuzo za muziki zinazolenga kutambua na kuenzi ubora wa wasanii wa Afrika katika nyanja mbalimbali za muziki zikiwa na kusudio la kukuza vipaji na kuunganisha muziki barani humo.

Mbali na hilo hulenga kuendeleza ubunifu wa muziki wa Kiafrika, kuongeza mvuto wa muziki huo kimataifa na kutoa fursa za kibiashara na ufadhili kwa wasanii kutoka barani humo.

Mwaka huu tuzo hizo zilihudhuriwa na wasanii wakubwa akiwemo Rema ambaye pia aliibuka msanii bora Afrika Magharibi, ilhali msanii wa Bongo Fleva, Juma Mussa maarufu Juma Jux ambaye licha ya kuibuka na tuzo ya Best Male Artist in East Africa, uwepo wake ulikuwa kivutio katika sherehe hizo zilizofanyika Lagos, Nigeria.

Katika sherehe hizo, Jux alikuwa anawania tuzo ya Msanii Bora wa Kiume wa Afrika Mashariki pamoja na Diamond Platnumz, Marioo, Mbosso kutoka Tanzania, Bein wa Sauti Sol (Kenya), Element Eleeeh na Bruce Melodie (Rwanda), Joshua Baraka (Uganda), Sat-B (Burundi) na Yared Negu (Ethiopia).

JU 04

Itakumbukwa mwaka jana ulikuwa wa mafanikio kwa nyota huyo baada ya kuchukua tuzo ya The Headies kama Msanii Bora wa Kiume na alipafomu kwenye tuzo hizo zilizotolewa nchini humo.

The Headies ni tuzo za muziki wa Nigeria zinazotambua na kuenzi ubora wa wasanii wa muziki wa Nigeria na Afrika pia. Zilianzishwa 2006 na Hip Hop World Magazine na zinajulikana pia kwa jina la Hip Hop World Awards kabla ya kubadilishwa kuwa The Headies.

Mwanaspoti linakuletea mambo yaliyomfanya Jux kunyakua tuzo ya Afrima mwaka huu.

JU 01

NDOA

Sababu kubwa inayotajwa kumpa mafanikio ni baada ya kumuoa binti wa muigizaji maarufu wa Nigeria, Iyabo Ojo, mwaka jana jina lake linaendelea kutajwa zaidi katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini Nigeria.

Umaarufu wa familia hiyo katika tasnia ya filamu na burudani ya Nigeria umechangia kwa kiasi kikubwa Jux na kumpa mwanga, huku mashabiki wa Nollywood wakianza kumtambua si tu kama msanii kutoka Tanzania, bali kama sehemu ya familia maarufu inayoheshimika katika burudani za Nigeria.

Ndoa hiyo haikumbadilisha Jux kimuziki tu lakini imeongeza mashabiki wengine wa kazi zake kwa idadi kubwa jambo lilimfanya kuwa na ushawishi kwa kipindi kifupi.

JU 03

TAMASHA LA NIGERIA

Mbali na mahusiano ya kifamilia, Jux anakuwa msanii wa kwanza kuandaa tamasha la muziki Nigeria la Juma Jux in Lagos na kupata mapokezi makubwa.

Kwenye tamasha hilo pia Jux alimpandisha Diamond Platnumz wakaimba pamoja wimbo wa Enjoy na wasanii wengine kutoka Nigeria akiwemo Phyno.

Tamasha alilofanya nchini humo, iliyovuta idadi kubwa ya mashabiki inaelezwa ni ushahidi wa wazi kuwa msanii huyo sasa ana soko lake nchini Nigeria.

Jux alionyesha utofauti mkubwa kuanzia kwenye maandalizi ya tamasha hilo na namna alivyopafomu jambo linaloonyesha ni wazi familia yake imembadilisha kwa kiasi kikubwa.

Kwa walioanza kumfuatilia Jux tangu anaanza muziki, kwenye majukwaa sio mzuri wa kucheza lakini kwa sasa ni kama amebadilika na anaimba na kutoa burudani ya kucheza jukwani.

Shoo hiyo imekuwa gumzo miongoni mwa wadau wa muziki wa Afrika Magharibi, ikionyesha Jux si msanii wa R&B pekee bali anauwezo wa kubadilika na kuimba Afrobeat.

JU 02

KOLABO NA MASTAA WA NIGERIA

Ushirikiano wake na wasanii wakubwa wa Nigeria, akiwemo Phyno, Ekunrawo ni moja ya sababu zilizotajwa kuwa nguzo muhimu katika safari yake ya sasa.

Kolabo hizo zimeongeza thamani ya muziki wake kwenye soko la Nigeria, huku zikimuweka Jux karibu zaidi na wasanii na watayarishaji wenye ushawishi mkubwa barani Afrika.

Kupitia kolabo hizo, Jux ameunganisha ladha ya R&B ya Kiafrika na midundo inayopendwa zaidi Nigeria, jambo lililoongeza kukubalika wa kazi zake kwa hadhira.

Ukiangalia hata kolabo alizofanya zina utofauti mkubwa mfano Halima, See Body na Majo alizofanya peke yake zinaonyesha namna Jux anavyounganisha utamaduni wa muziki wa nchi mbili Bongo Fleva na Afrobeat.

JU 05

AFRIMA YATAMBUA

AFRIMA si tu hutazama historia ya msanii, bali pia mwelekeo na kile alichokifanya kwa wakati husika. Umaarufu unaokua kwa kasi wa Jux Nigeria, ushiriki wake katika matamasha, kolabo na uwepo wake katika vyombo vya habari, umeelezwa kuwa sehemu ya vigezo vilivyompa nafasi ya kung’ara katika tuzo hizo.

Ushindi wake unaonekana kwa kile alichokifanya hivi karibuni, yanayomfanya Jux kuonekana kama msanii wa kimataifa.

Kwa Jux, tuzo ya AFRIMA si tu pongezi ya kazi yake ya muda mrefu, bali ni uthibitisho kuwa mlango wa Nigeria ni moja ya masoko makubwa ya muziki Afrika.

Kutoka kutambulika kawaida hadi kuwa jina linalokuwa, safari yake inaonesha namna mchanganyiko wa maisha binafsi, mikakati ya kazi na ushirikiano wa kisanii unavyoweza kumbadilisha msanii katika soko la kimataifa.


MSIKIE MWENYEWE

Akizungumzia mafanikio hayo, Jux anasema; "Ni kitu kizuri sana, inatupa nguvu kama tasnia ya burudani Afrika Mashariki kuonekana tunatambulika. Shoo ilikuwa kubwa na nilikuwa na hofu kidogo kwa sababu ya ugeni lakini nilijaribu kufanya kwa uwezo wangu naamini mwaka huu utakuwa na shoo za nyingi za aina ile."