Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Khadija Kopa avunja ukimya madai ujauzito wa Zuchu

Muktasari:

  • Hata hivyo, mama yake amevunja ukimya juu ya madai hayo akisema kwanza hana habari za ujauzito huo, lakini pia Zuchu hakai nyumbani kwake, huku akimalizia kwa kusema kwa kuwa ana mume, ujauzito si jambo la ajabu na kama upo utaonekana.

BAADA ya kusambaa kwa taarifa zinazodai msanii wa Bongo Fleva, Zuhura Othman Soud maarufu Zuchu kunasa ujauzito, imeelezwa kuwa mrembo huyo amekuwa akijificha nyumbani kwa mama yake, Khadija Kopa ili kukwepa wageni na watu wa karibu wa mume wake, Diamond Platnumz, wanaoingia mara kwa mara nyumbani kwake.

Hata hivyo, mama yake amevunja ukimya juu ya madai hayo akisema kwanza hana habari za ujauzito huo, lakini pia Zuchu hakai nyumbani kwake, huku akimalizia kwa kusema kwa kuwa ana mume, ujauzito si jambo la ajabu na kama upo utaonekana.

Mwanaspoti limetonywa na mtu wa karibu wa Zuchu kuwa licha ya kuwepo kwa taarifa hizo, msanii huyo amekuwa akijitahidi kulinda faragha yake kwa kipindi hiki, huku akidaiwa kutotaka kuweka wazi jambo hilo mapema.

Chanzo hicho kilidai kuwa, Zuchu amekuwa akikwepa mapaparazi pamoja na kupunguza kuonekana hadharani kwa hofu ya kuharibu sapraizi yake kabla ya muda muafaka.

“Si unajua Zuchu tangu atambue kuwa ana ujauzito alikuwa hapendi kuonesha kwamba anao na ndiyo maana alikuwa kimya kujibu madai ya wanamitandao kuhusu hilo na wala haposti picha mpya kama tulivyomzoea,” kilisema chanzo hicho.

Katika siku za hivi karibuni, mashabiki wa mwanamuziki huyo wamekuwa wakijiuliza kuhusu ukimya wake mitandaoni pamoja na kupungua kwa picha na video mpya tofauti na ilivyozoeleka awali.

Akizungumza na Mwanaspoti, Khadija Kopa alisema: “Embu niache mie, kwanza sina habari kwamba Zuchu ni mjamzito, na ujauzito nao ni wa kuficha? Wakati ni jambo la kheri. Mimi simuoni hapa nyumbani, muulizeni mume wake. Kwanza cha ajabu ni nini kama akiwa mjamzito? Si ana mume yule? Kama ipo mtaiona tu hakuna kificho,” amesema Khadija Kopa.

Taarifa zilieleza kwamba, Diamond na Zuchu walifunga ndoa mwanzoni mwa mwaka 2025 katika hafla iliyofanyika kimya kimya, jambo lililozua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kipindi hicho.