Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Keisha: Sirudi ng'o Tip Top

Na Mwandishi Wetu BAADA ya kupigwa 'stop' kutokanyaga Manzese ambako Kundi la Tip Top Connection limeweka makazi yake, mwanamuziki Keisha amesema kamwe hatarejea tena kundini humo. Keisha, ambaye jina lake halisi ni Khadija Shaban amesema hakukurupuka kuondoka katika kundi hilo na kusema uamuzi huo aliufanya baada ya kuona hahitaji kuendelea kuwepo. "Si kwamba nililala na kuamua asubuhi kuwa najitoa Tip Top, ni muda mrefu nimelifikiria hili, kwa hiyo watu wasijisumbue kufikiria labda ipo siku nitarudi, hiyo hutokea kama mtu hukujipanga. Ni muda mrefu nimekuwa nikipata maudhi ya hapa na pale, lakini nilivumilia ili nijipange namna nitakavyoendelea na maisha nikiwa 'kimpango' wangu, nimeshajipanga na sasa msubiri Keisha mpya nje ya Tip Top", alisema. Wiki iliyopita kiongozi wa kundi hilo, Hamis Taletale alitoa msimamo na kusema kuwa kamwe hawatampokea tena msanii huyo iwapo atataka kurejea kundini. Tale alisema: "Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyu kuondoka kundini, aliwahi kufanya hivyo mwaka 2008 lakini alirejea, walimkubalia wakiamini ni utoto unamsumbua." Kiongozi huyo alisema kundi halitafanya hivyo tena, kwani safari hii ameondoka bila kuaga na habari zake amekuwa akizisikia tu kwenye vyombo vya habari. "Hakuniaga naaamini hatakuja kuniomba msamaha tena, asije kufikiria kufanya hivyo kwani nafasi yake haipo tena namtakia kila la heri huko aendako," alisema Tale.