Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jihan atarajia mapokezi ya kifalme

MISS Pict
MISS Pict

Muktasari:

  • Baada ya kutwaa taji hilo Oktoba 10, 2026, jijini Bangkok, Thailand, sasa macho yanaelekezwa kwenye kurejea kwake nyumbani kesho Oktoba 17, 2026.

UJUMBE wa malkia mpya wa Miss Grand International 2026, Jihan Dimack, kwa Watanzania unasikika kama mwaliko wa sherehe kubwa inayosubiriwa kwa hamu. “Uwanja wa ndege. Nawapenda na ninatamani sana kuwaona nyote!” ni maneno yake yanayoongeza hamasa ya kumpokea binti huyo aliyetangaza nchi ya Tanzania katika jukwaa la kimataifa la urembo.

Baada ya kutwaa taji hilo Oktoba 10, 2026, jijini Bangkok, Thailand, sasa macho yanaelekezwa kwenye kurejea kwake nyumbani kesho Oktoba 17, 2026.

Lakini nyuma ya taji hilo yupo mtu mwenye nafasi kubwa katika ulimwengu wa mashindano ya urembo, Nawat Itsaragrisil, ambaye jina lake limekuwa sehemu ya mafanikio na mijadala inayozunguka Miss Grand International.


MIS 03

NAWAT, NI NANI

Nawat ni mfanyabiashara na mtangazaji kutoka Thailand, anayefahamika zaidi kama mwanzilishi na Rais wa Miss Grand International (MGI). Kabla ya kujikita kwenye mashindano ya urembo, alijijengea jina kupitia vipindi vya televisheni vilivyohusu safari na utamaduni.

Uzoefu huo ulimfungulia milango ya kuingia katika tasnia ya urembo, ambako baadaye aliamua kujenga jukwaa lake badala ya kubaki nyuma ya pazia.


MIS 04

MWAKA 2013 UKAWA MWANZO

Nawat alianzisha Miss Grand International mwaka 2013, akilenga kuifanya kuwa mashindano yanayovuka mipaka ya nchi na kuwapa warembo nafasi ya kujitangaza kimataifa.

Tangu wakati huo, MGI imeendelea kukua kupitia mashindano ya kila mwaka, ushiriki wa mataifa mbalimbali na shughuli za kibiashara zinazozunguka chapa hiyo. Kwa Nawat, mashindano hayahusu taji pekee, bali pia namna ya kujenga jina la mshindi na kulitumia kutengeneza fursa.


MIS 02

UREMBO UNAOKUTANA NA BIASHARA

Moja ya mambo yanayoitofautisha MGI ni kuhusisha mashindano na shughuli za kibiashara, ikiwamo matangazo, bidhaa na matukio ya kimataifa.

Kupitia mfumo huo, warembo wanaoshinda hupata nafasi ya kushiriki shughuli zinazoweza kuongeza mwonekano wao na kuimarisha chapa zao binafsi. Hii ndiyo sababu nafasi ya Nawat haiishii kwenye kutangaza mshindi, bali inahusisha pia usimamizi wa shughuli zinazozunguka mashindano hayo.


MIS 05

EMMA ALITANGULIA, JIHAN ANASUBIRIWA

Mwaka 2025, Emma Mary Tiglao wa Ufilipino aliposhinda taji la MGI, alifanyiwa mapokezi yaliyohusisha paredi katika Makati City na baadaye Pampanga, eneo alikokulia.

Tukio hilo lilionyesha namna ushindi wa kimataifa unavyoweza kugeuzwa kuwa sherehe ya nyumbani, inayompa mshindi heshima na kuongeza mwonekano wa mashindano husika.

Kwa Jihan, matarajio ya mapokezi makubwa yanaongezeka kutokana na ushindi wake unaoipa Tanzania nafasi ya kujitangaza katika jukwaa hilo. Ukubwa wa paredi na ushiriki wa Nawat vinategemea ratiba rasmi ya waandaaji wa mapokezi yake.


TANZANIA YASUBIRI MALKIA WAKE

Ujumbe wa Jihan umeongeza shauku ya mashabiki wanaotaka kumuona malkia wao akirejea na taji la kimataifa. Ikiwa mapokezi yataandaliwa kwa kiwango kikubwa itakua nafasi ya kusherehekea ushindi wake na kuitangaza Tanzania kwa  upana zaidi.

Macho yanaelekezwa kwenye kurejea kwa Jihan na mafanikio yake baada ya kutwaa taji hilo. Safari yake haimalizikii Bangkok ndiyo kwanza inaanza katika ukurasa mpya wa uwakilishi wa Tanzania na kimataifa kwenye ulimwengu wa urembo.