Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JET LI: Baada ya msoto, sasa anakula maisha

JET Pict

Muktasari:

  • Makala haya yanachambua kwa kina utajiri wa Jet Li, inavyoonyesha jinsi anavyopata kipato chake, anavyotumia, mchango wake kwa jamii, maisha yake binafsi pamoja na familia.
  •  

BEIJING, CHINA: WAIGIZAJI wengi wana stori zao tofauti juu ya kule walikotokea. Li Lianjie ambaye jina lake maarufu ni Jet Li ni miongoni mwa waliotokea katika mazingira magumu akizaliwa na wazazi waliokuwa na kipato cha chini sana.

Hata hivyo, juhudi na kipaji chake vimesababisha kuwa mmoja wa waigizaji 50 matajiri zaidi duniani hadi kufikia sasa.

Makala haya yanachambua kwa kina utajiri wa Jet Li, inavyoonyesha jinsi anavyopata kipato chake, anavyotumia, mchango wake kwa jamii, maisha yake binafsi pamoja na familia.

JET 01

ANAPIGAJE PESA

Anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 250 milioni. Chanzo chake kikuu cha mapato ni pesa anazolipwa kutokana na filamu na kijumla ameshiriki katika filamu zisizopungua 40, zikiwemo zile maarufu kama Shaolin Temple (1982), Once Upon a Time in China (1991), Romeo Must Die (2000), The One, Kiss of the Dragon, Hero, Fearless, The Expendables series (pamoja na Sylvester Stallone, Jason Statham, nk.)

Inaelezwa kwa kila kipande anachoigiza huwa anapokea zaidi ya Dola 1 milioni, kama ilivyokuwa katika The Expendables na alilipwa zaidi ya Dola 10 milioni kwa kipande alichoonekana.

Mbali ya pesa za filamu, Jet Li amekuwa balozi wa bidhaa mbalimbali za kimataifa, kama vile, Rolex (saa), Red Bull China, Uniqlo (mavazi), Tissot Watches ambazo zote kwa pamoja zinakadiriwa kumpa Dola 30 milioni kwa mwaka lakini baadhi ya kampuni hizo kwa sasa hafanyi nazo kazo.

Vilevile ana kampuni yake inayojihusisha na uzalishaji wa maudhui ya filamu barani Asia na mara kadhaa ameonekana akiwa mtayarishaji wa filamu mbalimbali.

JE 03

NDINGA

Bentley Continental GT        Dola 250,000      

Mercedes-Benz S-Class         Dola 120,000      

Range Rover Autobiography Dola 150,000      

Tesla Model S (kwa mazingira)       Dola 100,000      

JE 04

MIJENGO

Jet Li anamiliki nyumba za kifahari China na Singapore.

Nyumba yake ya kifahari ya  Singapore ina thamani ya zaidi ya Dola 20 milioni. Alihamia nchini humo mwaka 2009 baada ya kupata uraia wa Singapore.

Vilevile anamiliki nyumba maeneo ya Hong Kong na Beijing ambazo zote kwa pamoja zinakadiriwa kuwa na thamani ya Dola 40 milioni.

JE 02

MSAADA KWA JAMII

Jet Li si tu msanii bali pia ni mfadhili na mwanaharakati wa misaada ya kibinadamu. Mwaka 2007, alianzisha taasisi yake One Foundation inayojihusisha na misaada wakati wa maafa, elimu, afya ya akili na watoto.

Baadhi ya mafanikio ya taasisi yake  ni kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi la Sichuan (2008), Msaada kwa waathirika wa mafuriko kusini mwa Asia, kusaidia shule za vijijini kwa vifaa vya kujifunzia.

Hadi kufikia sasa Jet Li ametoa zaidi ya Dola 50 milioni kusaidia miradi ya kijamii kupitia One Foundation.

JE 05

BATA NA FAMILIA

Jet Li amewahi kuoa mara mbili. Mke wake wa sasa ni Nina Li Chi aliyewahi kushiriki mashindano ya urembo, pia alikuwa mwigizaji. Ana watoto wa kike wanne.

Watoto wake wote wanasoma katika shule binafsi za kimataifa na ameweka maisha yao nje ya kamera kwa lengo la kuwalinda.