Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jamani msikieni Kassim Mganga

MWANDISHI WETU HAKUNA cha Ally Kiba, Diamond wala Dully Sykes. Kassim Mganga wa Tiptop Connection amedai eti hakuna msanii wa kumfunika Bongo kwa kuimba nyimbo za mapenzi. Kassim ambaye ameachia ngoma yake ya 'Tajiri wa Mahaba' alisema; "Hakuna ubishi, mimi naimba nyimbo za mahaba na nadhani ninafanya vizuri sana na ndio maana hata mashabiki wangu wanavutiwa na kazi zangu, na si kwamba nilikuwa kimya kwa muda mrefu, bali nilikuwa chimbo nikiandaa kazi zenye kuwapa burudani mashabiki wangu." Kassim ambaye anatokea Mkoa wa Tanga, alisema kuwa tatizo la wanandoa wengi ambao wanaoana wamekuwa wakishindwa kutimiza yale waliyowaahidi wapenzi wao kabla ya kuoana na hatimaye ndoa nyingi sasa zimekuwa zikivunjika.