Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya kurudia nguo, Idris avunja ukimya

IDRIS Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Idris alisema hakupendezwa na swali la mwandishi wa habari wa media moja aliyemchomekea hivi karibuni kuhusu kurudia nguo, kwani kwa mtazamo wake wala sio tatizo.

MCHEKESHAJI Idriss Sultan amemwaga povu kwa watu waliomshupalia amekuwa akirudia nguo baada ya kumshtukia hivi karibuni.

Akizungumza na Mwanaspoti, Idris alisema hakupendezwa na swali la mwandishi wa habari wa media moja aliyemchomekea hivi karibuni kuhusu kurudia nguo, kwani kwa mtazamo wake wala sio tatizo.

“Binafsi sioni tatizo kurudia nguo, ila watu wanaongea kwa sababu mimi ni staa, niwaombe tu mashabiki zangu tufuatilie kazi na siyo mambo yasiyo na maana,” alisema mshindi huyo wa Big Brother Africa (BBA-Hotshots Edition) - 2014 na kuongeza;

“Na yule mwandishi ameniletea habari za watu wa mitandaoni kuniuliza mimi, hivi kweli unawezaje kuwafuatilia watu wa mitandaoni ikiwa kila wakiamka wana akili zao tofauti kichwani? Yaani huku ni kukosa kazi hadi kumfuatilia mtu mavazi, leo amevaa nini na kesho nini, hii  ni upuuzi kabisa.”