Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ines Raguel na ndoto za Grammy

INES Pict

Muktasari:

  • Mwanamuziki huyo ana ndoto ya kufika kwenye majukwaa makubwa ya kimataifa na kuwania tuzo za kifahari duniani, ikiwemo Grammy, huku safari yake ya muziki ikianzia kwenye kwaya za kanisani akiwa na umri wa miaka 14.

INES Raguel ni miongoni mwa wanamuziki wanaotaka kuleta utofauti katika muziki wa Afrika Mashariki kwa kutumia lugha ya Kifaransa, akilenga kujenga jina lake ndani na nje ya Tanzania.

Mwanamuziki huyo ana ndoto ya kufika kwenye majukwaa makubwa ya kimataifa na kuwania tuzo za kifahari duniani, ikiwemo Grammy, huku safari yake ya muziki ikianzia kwenye kwaya za kanisani akiwa na umri wa miaka 14.

Tofauti na wasanii wengi wanaojikita zaidi katika Kiswahili, Ines anaamini muziki wa Kifaransa unaweza kuwa sehemu muhimu ya safari yake ya kisanii. Akiwa na asili ya Tanzania, Burundi na Ufaransa, anasema ameamua kutumia mazingira aliyokulia na uwezo wake wa lugha kama fursa ya kujitofautisha katika muziki.


INE 01

KIFARANSA SILAHA YAKE

Ines baba yake ni Mtanzania na mama Mburundi, alizaliwa Ufaransa, baadaye akaishi Burundi kabla ya kuhamia Tanzania.

Historia hiyo imempa nafasi ya kufahamu tamaduni tofauti na kuutumia vizuri ulimwengu wa lugha ya Kifaransa katika muziki wake.

Akieleza sababu za kuchagua kuimba kwa lugha hiyo, anasema “Mimi ninaimba Kifaransa kwa sababu cha kwanza nakijua, pili nilijiuliza kwa nini nisiweze kufanya muziki wa Kifaransa hapa Afrika Mashariki wakati nakijua?”

Kwa mtazamo wake, muziki wa Kifaransa una nafasi ya kukua katika ukanda huu na anaamini anaweza kuitumia nafasi hiyo kujenga jina lake zaidi kwani anafahamu safari hiyo inahitaji kazi, uvumilivu na ubunifu ili kuifikia hadhira kubwa.


INE 02

KWAYA ILIMFUNGULIA NJIA

Ines alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 14 katika kwaya za Kanisa Katoliki na kushiriki katika sherehe mbalimbali za kanisani.

Hatua hiyo ilikuwa mwanzo wa safari iliyomsaidia kuzoea jukwaa na kuendeleza kipaji chake na baadaye, alianza kuimba katika shughuli za karaoke, alikoendelea kujifunza kupitia nyimbo za wasanii wengine.

Kadiri muda ulivyosonga, hamu ya kufanya muziki wake mwenyewe ilizidi kukua, akaamua kutoka kwenye kuimba nyimbo za wengine na kuanza kutoa kazi zake binafsi kupitia lebo ya Googlemanga Music.

Uamuzi huo ni hatua muhimu kwake, kwani sasa anajenga utambulisho wake na kutafuta namna ya kuwafikia mashabiki wanaopenda muziki wa aina tofauti.


INE 03

NDOTO ZA MAJUKWAA MAKUBWA

Ines hataki safari yake iishie kwenye kutambulika Tanzania pekee kwani anajiona akifika kimataifa, akitambulika kama msanii wa muziki wa Kifaransa kutoka Afrika Mashariki na kuwania tuzo kubwa duniani, ikiwemo Grammy.

“Miaka mitano ijayo najiona msanii mkubwa sana ambaye nina historia yangu kwenye muziki. Najiona kwenye majukwaa ya kimataifa, najiona nikileta tuzo,” anasema Ines.

Ni ndoto kubwa, lakini kwake ni sehemu ya malengo anayopaswa kuyafanyia kazi kila siku. Kwa sasa, anasema anaendelea na maandalizi ya EP yake mpya, ingawa bado hajaweka wazi tarehe ya kuitoa.

Kuhusu kushirikiana na wasanii wengine, anasema “Siku moja natamani kuwa kama Zuchu yeye ni role model wangu namfatilia sana style yake ya maisha ya muziki naamini nitafikia hata nuzu ya alipo kwa sasa.”