Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Heh! Matonya ameanza kufulia kweli

Matonya

MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM SIRI imefichuka kwamba Matonya ameuza nyumba yake ya jijini Tanga, lakini amewaambia marafiki zake wa karibu kwamba amefanya hivyo ili mambo yaende sawa kimaisha na siku si nyingi ataibukia kwingine. Staa huyo aliyewahi kuvuma na nyimbo kama 'Anita' na 'Tax Driver' amekuwa akijaribu kurudi kwenye chati ya muziki bila mafanikio ingawa habari zinasema ameamua kujihusisha na biashara zingine. Pamoja na rafiki zake kudai alikuwa akisoma kozi fupi ya kompyuta, lakini wamedokeza kuwa msanii huyo ameuza nyumba ili kupiga dili zingine na huenda akaanza kujenga tena baadaye mwaka huu. Kwa mujibu wa marafiki hao wa karibu, msanii huyo aliwaambia; Nimeuza na natumia hizo pesa kujenga nyumba nyingine, halafu nashindwa kuelewa hata watu wamejuaje Msanii huyo hakuweza kupatikana kuzungumzia sakata hilo kwa madai kuwa anaandaa mipango ya shoo zake za Ulaya.