Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fanya hivi muziki wako uteke hisia za mashabiki

HISIA Pict

Muktasari:

  • Kwa aslimia kubwa mashabiki hasa wa kizazi cha sasa kuna mambo yanawavutia hasa vaibu la wimbo na si kama wa miaka ya nyuma ambao walijali zaidi ujumbe kusikiliza neno kwa neno.

MUZIKI kama sanaa ina watu wake, fanani na hadhira. Fanani kwa maana ya mtunzi na mwimbaji na hadhira kwa maana ya mashabiki au wasikilizaji wa kazi zao.

Hata hivyo, kuna mambo ambayo kama msanii hatayazingatia, ni ngumu kwa kazi zake kufanya vizuri.

Wapo wasanii waliotoa nyimbo chache na kufanya vizuri na wale waliotoa kazi nyingi lakini hazijafika walikotaka.

Kwa aslimia kubwa mashabiki hasa wa kizazi cha sasa kuna mambo yanawavutia hasa vaibu la wimbo na si kama wa miaka ya nyuma ambao walijali zaidi ujumbe kusikiliza neno kwa neno.

Kwa kizazi hiki cha teknoloji kuna mambo ya kuzingatia ili kumfanya msanii kazi zake zifike mbali kwa kizazi cha Gen Z.

HISI 01

IWE RAHISI KUKARIRI

Kwanza wimbo lazima uwe na sehemu inayokaririka kwa haraka mwanzo wake usiwe mrefu (intro) ili iwe rahisi kukaa kwenye akili za mashabiki waliyokusudiwa kusikiliza nyimbo hizo.

Pia lazima kiitikio kiwe rahisi kuimbika kwa kutumia lugha rahisi na maneno machache, mfano mzuri ni nyimbo za Diamond Platnumz ya ‘I'm So Happy’ na ‘Komasava’ aliyoshirikiana na Jason Derulo na Khalil Harisson & Chley.

Pia kuna nyimbo kama ‘Hakuna Kulala’ ya Juma Nature, ambao una miaka mingi lakini bado una vaibu kwa sababu kiitikio chake ni rahisi kuimbika.

Mr Blue  ana wimbo wa Mapozi unaimbika kirahisi na unaeleweka , huku Mbosso na wimbo wake wa ‘Sele’ unatesa kwa sababu hiyo na nyingine nyingi za viitikio vya aina hiyo.


HISI 02

UBORA WA SAUTI

Utayarishaji wa muziki lazima uzingatie kuunda biti kurekodi kupanga vyombo/sauti (Production) uchang anyaji wa sauti kama kusawazisha voko vyombo vya muziki kama gitaa kinanda ngoma violini (instruments) sauti (volume) hivyo vyote vinatakiwa vipangiliwe vizuri ili kujenga ushawishi mkubwa kwa mashabiki.

Jambo lingine la msingi ni usawazishaji wa masafa ya sauti (EQ) efekti za sauti (Mixing) na uboreshaji na ukamilishaji wa sauti mfano kuifanya nyimbo iwe na sauti iliyokamilika yenye uwiano na kiwango kinachofaa kwa platfomu (Mastering).


HISI 03

FIKIRIA CHALENJI

Wakati unatengeneza wimbo  lazima kufikiria kipande ambacho kitatumika kwenye video ambazo mashabiki wanaweza wakatumia katika chalenji katika mitandao ya kijamii.

Ukuaji wa sayansi na teknolojia unawalazimisha wasanii kujua watumiaji wa mitandao wana staili gani ya maisha, mfano wa TikTok, Instagram na mingineyo ili kuwafanya kuwa sehemu ya kuutangaza wimbo.

Katika wimbo viwepo vionjo vya mahusiano ucheshi ambavyo asilimia kubwa vinafuatiliwa zaidi mitandaoni.Jambo lingine mwanamuziki hatakiwi kulazimisha watazamaji (viewers) na wafuasi (followers) bandia wanapaswa kuwa halisi watakaomsaidia kujua ni aina gani ya ujumbe wanaoupenda zaidi.


HISI 04

ISHU YA MAUDHUI

Wakati wa kutoa nyimbo pia kuwepo na kontenti za kutosha mfano ‘clip’ zinazotokana na wimbo ambao utawaandaa kuwa tayari au kuwapa hamu mashabiki kupokea ujio mpya wa kazi.

Mfano tengeneza nyingi kutoka kwenye wimbo huo anaweza akawa anaimba akiwa studio kwa video hasa sehemu kali ya wimbo wake na inayochezeka, pia msanii anaweza akawa anatumia waandaaji wa maudhui ili kuitangaza nyimbo yake.

Pia msanii anapaswa kufuatilia mapokeo ya jamii pale anapoona kipande cha wimbo wake kimependwa zaidi ili kuongeza nguvu eneo hilo kuliko kukimbilia kuachia baki tu baki.


HISI 05

UTAMBULISHO WA MSANII

Mwanamuziki anatakiwa kuwa na muonekano utakaomtambulisha kwa mashabiki wake ili kuvuta kwenda kuusikiliza wimbo wake, pia anapaswa kujibu ujumbe anaotumiwa ili kuonyesha yupo pamoja nao.


HISIA

Nyimbo ya msanii iwe na ujumbe wenye hisia zinaweza zikawa za kugusa mahusiano maisha mfano ule wa 20 Percent wa Maisha ya Bongo ,msanii Click Master na wimbo wa Watajua, unaozungumzia maisha namna ambavyo alivyopoteza watu na vitu ndipo akapata watu wengine na vitu vingine lakini kiwepo kipengele kinachoweza kuchezeka kwa upekee.


KAULI ZA WASANII

Msanii wa Bongo Fleva Sarah Michael 'Phina' ni kati ya watu wanaofuatiliwa zaidi mitandaoni kutokana na staili ya nyimbo zake mfano wimbo wa Nakuamini aliyoshirikiana na Eni raia wa Nigeria mtengenezaji wa maudhui mtandaoni anazungumzia hilo.

"Nazingatia vitu vingi kuhakikisha nyimbo zangu zinakwenda vairol nafuatilia mashabiki wanataka nini ikiwemo maproduiza wazuri ambao watatengeneza kazi yangu iwe nzuri" anasema.

Mw ingine aliyechangia hilo ni msanii wa Bongo Fleva Mr Blue anasema:"Nazingatia vitu vingi nikitaka kuachia nyimbo natumia muda mrefu kuangalia kila kitu cha kiufundi kama kimekaa sawa ndiyo maana huwezi kuona natoa nyimbo kwa mazoea."