Dolly Parton: Safari ya miaka 60 ya mafanikio kwenye muziki
Muktasari:
- Januari 1967, Parton aliingia kwa mara ya kwanza kwenye chati za muziki wa country za Billboard kupitia nyimbo mbili alizozitoa chini ya Monument Records, Dumb Blonde na Something Fishy.
NEW YORK, MAREKANI; MWANAMUZIKI Dolly Parton ni miongoni mwa mastaa maarufu zaidi wa muziki wa country duniani amefariki dunia kwa ugonjwa wa saratani, huku safari yake ya muda mrefu ikiendelea kuwa na mafanikio makubwa. Hizi ni baadhi ya hatua muhimu zilizotengeneza historia ya mwanamuziki huyo.
Parton aliandika na kutoa wimbo wake wa kwanza, Puppy Love, akiwa na umri wa miaka 11 kupitia lebo ya Goldband Records. Wimbo huo uliambatana na B-side uliokwenda kwa jina Girl Left Alone.
Ingawa wimbo huo haukuwa na mafanikio makubwa kibiashara, Parton alipata nafasi ya kutumbuiza kwa mara ya kwanza katika ukumbi maarufu wa Grand Ole Opry, Nashville, Tennessee, akiwa na umri wa miaka 13. Alitambulishwa na gwiji wa muziki, Johnny Cash.
Januari 1967, Parton aliingia kwa mara ya kwanza kwenye chati za muziki wa country za Billboard kupitia nyimbo mbili alizozitoa chini ya Monument Records, Dumb Blonde na Something Fishy.
Mwaka 1971, alipata wimbo wake wa kwanza kushika nafasi ya kwanza kwenye chati za country kupitia Joshua.
Miaka mitatu baadaye, mwaka 1974, wimbo wake maarufu Jolene ulifika kileleni mwa chati za muziki wa country, ukiwa miongoni mwa nyimbo zilizokuja kutambulisha zaidi jina lake duniani.
Mafanikio yake yaliendelea na mwaka 1975 alitwaa tuzo ya Female Vocalist of the Year katika tuzo za Country Music Association (CMA).
Mwaka 1978, wimbo wake Here You Come Again ulipata hadhi ya platinum, huku albamu hiyo ikimzawadia Parton tuzo ya Grammy ya Best Female Country Vocal Performance.
Mwaka 1980, Parton aliingia rasmi kwenye tasnia ya filamu alipocheza katika filamu yake ya kwanza, 9 to 5, pamoja na Lily Tomlin na Jane Fonda. Katika kipindi hicho pia alitoa wimbo wa jina hilo ambao ukawa miongoni mwa kazi zake zilizopata umaarufu mkubwa.
Mwaka 1986, Parton alifungua bustani yake maarufu ya burudani, Dollywood, iliyopo Pigeon Forge, Tennessee.
Baadaye mwaka huo, alitunukiwa heshima ya kuingizwa kwenye Nashville Songwriters Hall of Fame, akitambuliwa kwa mchango wake mkubwa katika utunzi wa nyimbo.
Akiwa na umri wa miaka 75, Parton alirejea kwenye kumbukumbu za mwaka 1978 kwa kuiga jalada lake maarufu la jarida la Playboy kama sehemu ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mume wake, Carl Dean.
Mwezi Mei 2022, ilitangazwa rasmi kwamba Parton angeingizwa kwenye Rock & Roll Hall of Fame, pamoja na mastaa wengine wakubwa akiwemo Eminem, Lionel Richie, Carly Simon, Eurythmics, Duran Duran na Pat Benatar.
Kutoka kuanza kurekodi muziki akiwa mtoto hadi kuwa mmoja wa majina makubwa zaidi katika historia ya muziki wa country, Parton amejenga urithi unaoendelea kudumu katika muziki, filamu na burudani.